Adeladius Makwega, DODOMA.
JANUARI 27, 2022 niliamka nyumbani kwangu kama zilivyo siku nyengine. Nilipofika kituo cha basi nilikutana na daladala ambayo nilipata kiti na kuketi na kuianza safari ya kuelekea huko kwa kina pangu pakavu tia mchuzi.
Daladala hiyo, abiria wake hatukuwa wengi sana lakini viti vyote vya basi hili vilijazwa.Tuliendea na safari kama dakika tano hivi, naye kondakta alipita na kuchukua pesa yake na mie kumlipa shilingi 1000 na kumuelekeza kuwa nimepanda Chamwino nashuka Mji wa Serikali.
Safari iliendelea, huku kwa mbali nikisikia katika redio kama sauri ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassani. Sauti hiyo nilibaini yupo katika kipindi kimojawapo cha TBC Taifa. Lakini baadaye nilitambua hakuwa TBC Taifa, bali alikuwa TBC 1. Hawa jamaa wa TBC Taifa niligundua kuwa walijiunga tu.
Huku nikiwa katika daladala hiyo nilibaini kumbe TBC 1 walikuwa na mheshimiwa Rais kwani mheshimiwa huyu alikuwa akisherehekea sikukuu yake ya kuzaliwa Januari 27.
Nikiwa katika basi hili niliona kila abiria yu kimya, tukisikiliza namna mheshiwa wetu akiongea. Binafsi nilikuwa kimya zaidi kusikiliza je kuna abiria yoyote atasema chochote juu ya siku ya kuzaliwa ya mheshimwa huyu?
Masikio na macho yangu yalikuwa kama mshabiki wa mpira ambaye timu yake imefungwa alafu timu yake inashambulia goli la adui.Nilikuwa kama shabiki aliyekodoa macho na kutega masikio yake kusubiri goli kuingia kimiani.
Lakini hilo sikulishuhudia mwanakwetu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...