Na Khadija Seif , Michuzi TV

MSANII Skales kutoka nchini  Nigeria ambaye tangu aingie kwenye tasnia Huu ni mwaka wake wa 12  ameongeza thamani kutoka kuwa Msanii Mdogo Mwenye Kipaji (talanta) mpaka kuwa icon wa afropop na orodha iliyojaa nyimbo nyingi ambazo zinafanya vizuri kwa kasi ya kimataifa. 

Baada ya kizuizi cha muda mrefu Nigeria kilichotekelezwa na COVID-19, alielekeza nguvu kwenye EP yake “Healing process EP” yenye mchakato wa uponyaji tafakari ,simulizi Za kufikirisha ambazo hakika zilimpeleka Hadi kwenye kilele cha taaluma yake.

Mwaka 2021 malengo yake makubwa yalikuwa nikurudi kwenye fomu ya kuunda nyimbo za pop ambazo zilimfanya kuwa juu katika Chati nyingi ndani na nje ya Nigeria. 

Nyimbo kama vile "Kayefi," ambayo ilihusu dhana ya kupata urafiki wa kimapenzi huku "This Your Body," wimbo aliomshirikisha Davido ulikuwa ni wimbo wa nadharia ya furaha ya mwili wa mwenzi. Pia , alitoa "I Dey Miss You," wimbo wa kuchezeka na ulifanya vyema. 

Skales 2022 , amekuja na “No body to Somebody” Ukiwa ni wimbo unaohadithia maisha yake na kuwapa Nguvu wale wote wanao tafuta bila mafanikio kuwa iko siku watafikia malengo Yao.

Maneno kadhaa kwenye wimbo huu ni ya nyimbo Za injili maarufu miaka ya 80, "Nobody 2 Somebody" Skales anaeleza namna anavyopitia  msururu wa hali ngumu ambazo anawahimiza wasikilizaji wake kuendelea kupigania ndoto zao na kufanya kazi zao ili kufaulu maisha yao.

Unaweza Sasa kuupata wimbo huu kupitia Platform zote Za kuuza nyimbo duniani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...