NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete amesema kuwa ameridhishwa na utekelezaji wa miradi ya Shirika la Nyumba la Taifa inayotekelezwa mkoani Arusha. 

Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete ameyasema hayo katika eneo la Mradi wa SafariCitywakati akihitimisha ziara yake ya siku mbili mkoani Arusha ambapo jana alishiriki kwenye ziara ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Majaliwa kwenye ukaguzi uliofanywa katika eneo la EPZA unapojengwa Mji wa Tanzanie katika Mji Mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro akiwa katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo mkoani Manyara. 

“Nimeridhishwa sana na maendeleo niliyoyaona kwenye miradi ya Shirika hapa Arusha na kama kuna changamoto mnazo mtufahamishe kama Wizara tujadiliane tuzitatue na mambo yaendelee wananchi wapate makazi bora, Mkurugenzi Mkuu ninakuamini wewe na wenzako kwa asilimia 100, chapa kazi kwa kuamininiana tusonge mbele,”amesema. 

Amekaribisha uongozi wa Shirika kuwasilisha mawazo yoyote yale chanya yatakayoweza kulisongesha Shirika mbele kwaajili ya mustakabali wa Shirika lakini pia mustakabali wa Taifa kwa ujumla. 

“Haya maeneo ya kimkakati iwapo yatatumika vizuri yataisaidia Serikali katika kupanga miji, mmefanya vizuri kuipanga miji hii simamieni utekelezaji wa mipango yenu ili tuwe na miji ya kisasa. 

Amemshukuru Mheshimiwa Rais kwa kusaidia Wizara kiasi cha shilling bilioni 50 za kupanga na kurasimisha ardhi na kuwataka viongozi wa ngazi za mikoa kuzisimamizi fedha hizo ili miji ipangike na kwamba wao kama Wizara watapita kusimamia utekelezaji.

“NHC jipeni muda wa kufikiria kuuza maeneo kwa kukata viwanja na au kuwauzia wenye uwezo wa kuendeleza maeneo hayo na mkifanya hivyo mtujulishe ili tuwe na maamuzi ya pamoja ili tumsaidie mheshimiwa Rais,” amesema. 

Amesema wao ndani ya Wizara tunakaribisha mawazo yoyote yale chanya yatakayoleta ufanisi wa Shirika na sekta ya nyumba kwa ujumla hata kama kwenye haya maeneo ya Shirika linataka kuuza maeneo na lina changamoto fulani fulani wafahamishwe watazitatua na mambo yatakwenda vyema. 

Amechukua fursa hiyo kumtakia Mheshimiwa Rais kwa kutimiza siku yake ya kuzaliwa na kumtakia afya njema na umri mrefu na hekima ya kuongoza Taifa. 

Kuhusu maombi ya kujengewa daraja litakalounganisha mji wa SafariCity na barabara ya Afrika Mashariki alisema ataliwasilisha suala hilo kwa TARURA na kwa Wizara husika ya TAMISEMI pamoja na Ujenzi.ili eneo hilo liweze kufikika kwa urahisi na kuliongezea Shirika na Taifa mapato. 

Naye Kaimu Meneja wa Shirika la Nyumba mkoa wa Arusha, Amani Tongora amesema kuwa utekelezaji wa mauzo ya mradi wa SafariCity unaenda viziuri na kwamba kimebaki kiasi kidogo cha makusanyo na mauzo yanayofanywa na Shirika kwa sasa pia amesema kuwa wananchi wamepewa miaka mitatu kukamilisha manunuzi ya viwanja huku hizi sasa kukiwa na punguzo la asilimia 40 la mauzo ya viwanja. 

Wakati huo huo jana Naibu Waziri wa Ardhi akiwa katika msafara wa Waziri Mkuu alisema Wizara ya Ardhi imejipanga kutatua migogoro mbalimbali inayolikabili Taifa na watalifanya hilo kwa njia shirikishi ya Mashirikiano na Wizara nyingine. 

Kabla ya kufanya ziara ya miradi ya Shirika la Nyumba la Taifa, Naibu Waziri alipata fursa ya kuzungumza na Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela juu ya masuala mbalimbali yanayohusu ardhi na utatuzi wa migogoro na hasa kuhusu maeneo ya wafugaji na kwenye mipaka ya hifadhi za taifa na namna ya kutatua matatizo.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Ridhiwani Kikwete akifuatilia maelezo ya Kaimu Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) mkoa wa Arusha, Amani Tongora alipokuwa katika ziara ya mradi wa SafariCity leo.

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Ridhiwani Kikwete akifuatilia maelezo ya Kaimu Mkurugenzi wa Shamba la Hortanzia wa kwanza kulia wakati alipotembelea eneo la USA River linalomilikiwa na NHC na kupangishwa kwa Hortanzia. 

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Ridhiwani Kikwete akiwa katika eneo la USA River. Eneo hilo la la USA River linamilikiwa na NHC na kupangishwa kwa Hortanzia. 
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Ridhiwani Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Arusha na Watendaji wa Idara ya Ardhi mkoa wa Arusha na watendaji wa NHC.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Ridhiwani Kikwete akitia saini kitabu cha wageni Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
 
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Ridhiwani akiwa eneo la Mirerani jana aliposhiriki kwenye ukaguzi wa Kituo cha Biashara ya Madini Mirerani kilichopo kwenye mji tarajiwa wa Tanzanite City kinachoanza kujengwa kwa kandarasi ya NHC kwa mwaka mmoja na nusu.
 
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Ridhiwani akiwa eneo la Mirerani jana alipotembelea eneo linapojengwa Kituo cha Biashara ya Madini Mirerani kilichopo kwenye mji tarajiwa wa Tanzanite City.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...