Waziri wa Katiba na Sheria George Simbachawene akizungumza na Menejimenti ya RITA wakati alipofanya ziara juu kuitambua ofisi hiyo na shughuli zake jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Mary Makondo akizungumza kuhusiana na RITA ambayo iko chini ya Wizara hiyo juu ya majukumu yake wakati wa ziara ya Waziri wa Katiba na Sheria George Simbachawene jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Khatibu Kazungu akizungunza wa wakati wa Mkutano wa ziara ya Waziri wa Katiba na Sheria George Simbachawene,jijini Dar es Salaam.
Kaimu Afisa Mtendaji wa Mkuu wa Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) Emmy Hudson akitoa taarifa za utendaji wa RITA kwa Waziri wa Katiba na Sheria George Simbachawene aliyefanya ziara katika ofisi za RITA jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Katiba na Sheria George Simabchawene akizungumza na menejimenti ya RITA alipofanya ziara katika ofisi hiyo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Katiba na Sheria George Simbachawene akiwa ameshika moja cheti sehemu ambayo vyeti vinachakatwa na RITA ,jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya RITA Profesa Khamis Henga akitoa taarifa ya Bodi kwa Waziri wa Katiba na Sheria George Simbachawene wakati alipofanya ziara katika ofisi hiyo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Katiba na Sheria George Simbachawene akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya RITA mara baada kufanya mazungumzo ya kiutendaji jijini Dar es Salaam.


*Kesi za mirathi na Taraka zinahitaji taarifa kwa haraka
*Hudson aahidi kwenda kwa kasi katika maboresho yanayokwenda wakati wa sasa.

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
WAZIRI wa Katiba na Sheria George Simbachawene ameitaka Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) kuimarisha kwa mfumo wa Tehama na Mahakama ili kuweza kusaidia katika masuala yote ya utoaji haki kwa wananchi ndani ya muda mwafaka.

Simbachawene ameyasema hayo hii leo Januari 27,2022 wakati alipofanya ziara katika ofisi za Wakala huo jijini Dar es Salaam, aidha amesema kuwa RITA ni Taasisi muhimu kwa nchi na hata katika kimataifa hivyo mifumo yake ya tehama itasaidia katika masuala ya ushahidi mahakamani pale inapohitajika kufanya hivyo na mifumo kutoa majibu mara moja badala ya kutegemea makaratasi kutoka ofisi moja kwenda nyingine.

Amesema kuwa kuna changamoto katika masuala ya talaka na mirathi ambapo kunahitajika kuwepo kwa taarifa katika mfumo wa kielektroniki pindi ikitokea pande mbili zinakizana kuhusu talaka au mirathi na suruhisho pekee ni mifumo ya TEHAMA ndiyo itajibu matakwa hayo na baadaye haki ikatendeka kwa tena kwa wakati wakati.

Waziri Simbachawene amesema kuwa RITA wasajili matukio yote kwani kuna baadhi watu wanafariki lakini taarifa zao hazipo washirikiane na wajumbe wa nyumba 10 ambapo watapata taarifa hata kama alifariki msituni.

Amesema watu wote wasajiliwe lakini kupata cheti ni hatua nyingine pamoja na kusajili matukio yote hapo itarahisisha serikali kuwa na taarifa za watu wake kwa ajili ya mipango mbalimbali ya maendeleo maendeleo.

Simbachawene amesema kuwa wanachi wanahitaji kuhudumiwa katika kufikia matamanio ya Rais Samia Hassan Suluhu kwa Tanzania anapoitaka iwe katika sura yenye watu wenye taarifa.

Aidha amesipongeza RITA kwa kuimarisha mifumo pamoja na kwenda kwa kasi katika usajili wa vyeti vya kuzaliwa.

Amesema kuwa RITA isajili watoto wote chini ya miaka mitano hadi wale wanaozalishwa na wakunga wa jadi.

Amesema RITA wamepiga hatua katika Ndoa na taraka kwa kipindi kifupi ambapo sasa mfumo wa ndoa umekuwa imara kwa kupata taarifa za ndoa kupitia taasisi za dini.

Hata hivyo changamoto za mirathi iko kwa matajiri na wale wenye kipato ambapo suluhisho lake watu wasajili wosia na kufanya watu wanaostahili wanapata haki.

Kwa upande wa Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu Emmy Hudson amesema kuwa kwa kipindi kifupi wamesajili Wosia 876 huku Wosia 70 zikichukuliwa na taraka 104 zimesajiliwa.

Amesema kuna changamoto watumishi katika ofisi hiyo kwa kuwa na watumishi 147huku mahitaji yakiwa 342 na kuendelea kufanya maboresho ili kuendana na wakati wa sasa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...