Na Said Mwishehe, Michuzi TV
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewaambia Mawaziri na Manaibu Mawaziri wote kuwa Januari 13 mwaka huu atakutana nao ili kuwafunda kabla ya kuanza kutekeleza majukumu yao.

Akizungumza baada ya kuapishwa kwa Mawaziri, Manaibu Mawaziri, Makatibu Wakuu, Manaibu Makatibu Wakuu pamoja na wateulie wengine , Rais Samia amesema leo sio siku ya kutoa hotuba kwa Taifa, hivyo mawaziri na manaibu mawaziri atakutana nao Januari 13 mwaka huu.

"Leo walisema nitahutubia Taifa lakini leo sitatoa hotuba yoyote, Mawaziri na Manaibu Mawaziri tutakutana Januari 13, tukikutana huko tutazungumza.Makatibu Wakuu na Manaibu Makatibu Wakuu nyie tutakutana kwa tarehe ambayo itapangwa lakini Januari 13 tutakuwa na Mawaziri na Manaibu Mawaziri tutakuwa pamoja, tutafungandana tukiwa ndani,wale wa sekta nyingine niwatakie kazi njema"amesema Rais Samia.

Kwa upande wake Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza kabla ya kumkaribisha Rais Samia, amewapongeza wote walioteuliwa na Rais kushika nafasi mbalimbali walizopangiwa.

"Ninyi mawaziri na manaibu mawaziri pamoja na mimi Rais ametuamini kumsaidia kazi, kama ambavyo Naibu Spika ameelekeza kazi zote zote ni za Rais lakini walioteuliwa wameamiwa kumsaidia, hivyo sote twendeni tukamsaidie kwa uaminifu na uadilifu mkubwa.Kuna majukumu mengi katika sekta zetu,"amesema Waziri Mkuu.

Ameongeza "Mheshimiwa Rais najua baada ya hapa ninayo fursa ya kukaa na mawaziri, makatibu wakuu na manaibu makatibu wakuu kwa ajili ya kuzungumza na kuweka mikakati ya kutekeleza vema majukumu yetu.Kwa niaba yao mawaziri wote, makatibu wakuu na manaibu makatibu wakuu kama baraza la kazi...

"Tukuahidi tutafanya kazi kazi kwa uaminifu mkubwa sana, tutafanya kazi kwa uadilifu mkubwa sana, Rais umekuwa ukisisitiza kufanya kazi kwa matokeo chanya, katika majukumu na mipango yetu tutafanya katika matokeo chanya, tutakwenda kusikiliza wananchi wa maeneo yote ya utekelezaji yatakuwa chanya."

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...