Waandaaji
wa Kilimanjaro Premium Lager Marathon wametangaza mdhamini mpya wa mbio
hizo, Surveyed Plots Company (SPC) Ltd ya Jijini Dar es Salaam ambayo
itatoa zawadi ya viwanja kwa mtanzania wa kwanza wa kiume na wa kike
katika mbio za km 42 za mwaka huu.
“Gharama
zote za kusajili viwanja hivyo kwa majina ya washindi zitagharamiwa na
kampuni ya SPC Ltd,”walisema waandaaji hao katika taarifa iliyotolewa
Jijini Dar es Salaam.
Mkuu
wa Uendeshaji wa kampuni ya SPC, Kenny Rodgers, alisema wanajivunia
kuwa sehemu ya mashindano makubwa ya Kilimanjaro Marathon 2022. “Hili ni
tukio kubwa na ni nafasi nzuri kwetu kujitangaza kwani haya ni
mashindano makubwa ya riadha katika ukanda mzima wa Afrika Mashariki na
hasa ikizingatiwa kuwa mashindanoi hayo yanaadhimisha miaka 20,”
alisema.
“Tutafanya utaratibu wa kuwamilikisha viwanja hivyo kwa majina yao na kuwapa nyaraka zote,” alisema Bw. Rodgers.
Alitoa
wito kwa watanzania wajifue na kujiandaa vizuri kwa mbio hizi za Km 42
ili wajishindie viwanja hivi. “Tunaamini ushindani utakuwa mkubwa kwa
hivyo watakaojiandaa vizuri wana nafasi kubwa sana ya kushinda mwisho wa
siku,” alisema.
Wadhamini wa mbio za Kilimanjaro Marathon 2022 ni Kilimanjaro Premium Lager (Mdhamini Mkuu) Tigo (21km) na Grand Malt (5km).
Wadhamini
wa meza za maji ni pamoja na Absa Tanzania, Unilever Tanzania, TPC
Sugar, Simba Cement na Kilimanjaro Water. Wasambazaji rasmi ni
GardaWorld Security, Keys Hotel, Kibo Palace Hotel, CMC Automobiles na
Surveyed Plots Company Ltd (SPC) na Bodi ya Utalii (TTB).
Katika
hatua nyingine, Kwa mujibu wa waandaaji wa Kilimanjaro Marathon, kwa
mara ya kwanza kutakuweko na maonesho yanayojulikana kama Kili Expo (The
People's Expo) ambapo wadhamini na wadau wengine wa mbio hizo watapata
fursa ya siku tatu za kuonyesha bidhaa na huduma wanazotoa, maonyesho
ambayo yanatarajiwa kufanyika kati ya Februari 24-26, 2022, katika
viwanja vya MoCU.
"Maonyesho
haya pia linakusudiwa kuwapa umma uzoefu wa muda mrefu wa mbio za Kili
Marathon; pia kwa mwaka huu wanaotarajia kushiriki mbio hizo watapata
fursa ya kuchukua namba zao za ushiriki eneo la chuo kikuu cha Ushirika
badala ya eneo la hotel kama ilivyokuwa miaka ya nyuma”, ilisema taarifa
hiyo ya wandaaji.
Mbio
za Kilimanjaro Premium Lager Marathon, zinatarajiwa kufanyika Jumapili
ya Februari 27, 2022, katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi
(MoCU), ambapo zimeandaliwa na taasisi ya Kilimanjaro Company Limited na
kuratibiwa na wadau wa hapa nchini kampuni ya Executive Solutions
Limited.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...