Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha

Katika utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya 2020-2025, fedha za miradi zilipokelewa kwa Mwaka 2021/2022 ,Halmashauri ya Mji wa Kibaha, Mkoani Pwani imepokea kiasi cha sh.Bilioni 53.8.

Kati ya fedha hizo sh.894,659,920 RUWASA sh.18,051,104.30,DAWASA sh.2,557,131,040 TARURA sh.1,097,822,898 na TANESCO sh.49,298,700,000 Jumla ikiwa ni sh.Bilioni 53.866.364.962.3.

Mkuu wa wilaya ya Kibaha, Sarah Msafiri, alieleza katika kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ,Halmashauri ya Mji Kibaha, mpaka kufikia robo ya pili ya Mwaka wa Fedha 2021/2022 kupitia vyanzo vyake vya ndani hadi kufikia tarehe 30 Disemba,2021 imeshakusanya sh.2,888,959,200 kati ya sh.4,107,012,000 sawa na asilimia 70.3.

Pamoja na hilo, alieleza kwamba, katika kutekeleza sekta ya Viwanda na Biashara ilani ya Chama cha Mapinduzi katika ibara ya 46 (g) inaelekeza juu ya kuandaa mikakati ya upatikanaji wa mitaji kwa ajili ya uanzishaji wa Viwanda vidogo vidogo, vya kati na vikubwa.

"Katika kutekeleza hilo, Halmashauri ya Mji Kibaha imefanikiwa kuendelea na ujenzi wa Viwanda 15 kati yake vikubwa ni 4,vya kati ni 9 na vidogo vidogo 2."

"Hadi kufikia Disemba jumla ya Viwanda vikubwa ni 28,vya kati ni 23 na vidogo vidogo ni 9"alifafanua Sarah.

Aidha ,Sekta ya Elimu Sekondari ibara ya 80 (I), Halmashauri imetekeleza ujenzi wa vyumba 47 vya Madarasa katika shule za Sekondari 13 baada ya kupokea milioni 940 za mpango wa Maendeleo wa ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO-19..

Sarah alisema, tayari Madarasa yamekamilika na yameanza kutumika tangu tarehe 17 Januari,2022.

"Katika kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwenye sekta ya afya ibara ya 83 (d)

Halmashauri ya Mji Kibaha imeanza ujenzi wa Kituo cha Afya Kongowe baada ya kupokea sh.250 milioni fedha za tozo kutoka Serikali kuu." hospitali ya Wilaya Lulanzi imeendelea kuboreshwa kwa kuongezewa majengo matatu ambayo ni wodi ya wanawake,wanaume na Watoto."

Mkuu huyo wa wilaya alibainisha kuwa, Mpaka Sasa yapo hatua ya ukamilishaji.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...