Na Amiri Kilagalila,Njombe.
 

Ili kuimarisha afya na kupambana na changamoto za kiuchumi kutokana na tatizo la ajira kwa vijana,kampuni ya Shikamoo Parachichi kupitia balozi wake ambaye ni msanii wa muziki wa bongo flavour mkoani Njombe maarufu kwa jina la B2K,wameanzisha ligi ya mpira wa miguu mjini Makambako kwa malengo makubwa ikiwemo kuhamasisha kilimo cha Parachichi.

Akizungumza na vyombo vya habari ofisini kwake mkurugenzi wa kampuni ya Shikamoo Parachichi iliyopo mjini Njombe bwana Erasto Ngole mara baada ya kutembelewa na balozi wa kampuni hiyo amesema.

“Tunavyo fanya hivyo kwanza tunaboresha afya za vijana,tunawaweka pamoja vijana lakini pia tunawafikishia meseji mbali mbali zikiwemo za ujasiriamali na kuwafundisha jinsi ya kujitegemea.Vijana wengi wapo mtaani na ni wasomi wazuri lakini ajira ni chache,tunachotaka vijana wa kitanzania wajue kujitegemea kutokana na mazingira wanayoishi”alisema Erasto Ngole

Aidha Ngole ambaye pia ni katibu wa siasa na uenezi mkoa wa Njombe,amesema fainali za michuano hiyo itakuwa ni siku ya tarehe tano mwezi wa pili katika uwanja wa amani Makambako siku ambayo ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapiduzi (CCM) na kubainisha kuwa ligi hiyo itaanza kufanyika kila baada ya miezi mitatu katika maeneo mbali mbali ya mkoa wa Njombe kwa udhamini wa kampuni ya Shikamoo Parachichi.

Kwa upande wake balozi wa kampuni hiyo ambaye ndiye mwanzilishi wa mashindano hayo bwana B2K amesema ligi hiyo iliyohusisha timu 12 inayoendelea mjini Makambako,mpaka sasa imefika mzunguko wa pili itakuwa na zawadi mbali mbali ikiwemo Ng’ombe,mbuzi na mpira.

“Pia tumeamua kuunga mkono vipaji na kupitia hii ligi pia tumebahatika kuna vijana wameenda Mbeya Kwanza kwa kuwa kuna watu wamekuja kuwaona wakati ligi inachezwa.Na sisi Shikamoo Parachcichi tutatoa zawadi ya Ng’ombe kwa mshindi wa kwanza,mbuzi wawili kwa mshindi wa pili na mpira mmoja kwa mshindi wa tatu”alisema B2K balozi wa Shikamoo Parachichi.

Vile vile ametoa wito kwa wakulima wa matunda ya Parachichi kuendelea kuunga mkono kampuni hiyo katika maswala mbali mbali ikiwemo ununuzi wa Parachichi kwa kuwa inafanya shughuli mbali mbali tangu walipoanza kuhamasisha kilimo hicho mwaka 2007 ili kujikwamua kiuchumi kupitia kilimo.

“Kwanza sisi ni wakulima tunaojihusiha na kilimo cha Parachichi lakini pia tunanunua Parachichi sehemu yeyote na kwa wakulima tofauti vile vile tunatoa elimu jinsi ya kulima na kuyatunza na tunauza hayo matunda pia nje na ndani ya Tanzania na ndio maana tunajiita Shikamoo Parachichi”aliongeza B2K

Mkurugenzi wa kampuni ya Shikamoo Parachichi bwana Erasto Ngole ametoa wito kwa wananchi wa mji wa Makambako kuendelea kujitokeza kwa wingi katika mashindano hayo ili kuheshimisha mashindano.

Mti wa parachichi uliohudumiwa vizuri na kutoa matunda pamoja na moja ya mkulima wa Parachichi mkoani Njombe akifurahia mavuno ya matunda

Kushoto ni msanii wa bongo Flavor mkoa wa Njombe maarufu kwa jina la B2K amabye ni balozi wa kampuni ya shikamoo Parachichi akipewa pongezi na mkurugenzi wa kampuni ya Shikamoo Parachichi Erasto Ngole kwa kuanzisha mashindano ya mpira mjini Makambako
Msanii B2K akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukutana na mkurugenzi wa Shikamoo Parachcichi ili kuzungumzia maswala mbali mbali ya ligi ya B2K CUP yanavyoendelea mjini Makambako
Erasto Ngole mkurugenzi wa shikamoo Parachichi akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelewa na balozi wa kampuni hiyo ofisini kwake.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...