Na Amiri Kilagalila,Njombe


Wakati Chama cha Mapinduzi CCM kikiendelea na maadhimisho ya miaka 45 ya kuzaliwa kwake kwa jumuiya zake kufanya shughuli mbalimbali,kivutio kikubwa kimekuwa ni zao la Parachichi kwa jumuiya hizo kuadhimisha kwa kuzipanda.

Wananchi wengi mkoani Njombe wamelekeza nguvu zao kwenye kilimo cha zao hilo ambapo jumuiya ya umoja wa wanawake Tanzania (UWT) wilaya ya Njombe chini ya mwenyekiti wake Beatrice Malekela wamelazimika kuadhimisha miaka 45 ya kuzaliwa kwa chama hicho kwa kupanda miche 110 ya parachichi katika kata ya Utengule katika halmashauri ya mji wa Makambako mkoani Njombe.

“Ekari moja tuliyoipanda tutaibuka kidedea yaani pale baada ya miaka mitatu kata ya Utengule tutakuwa tunazungumza habari nyingine na kila mchumo pale tunaweza kukuta tunavuna milioni nane”alisema Beatrice Malekela

Kwa niaba ya mbunge wa jimbo la Makambako aliyenunua miche hiyo,katibu wake Vasco Mgunda amewataka wana CCM wa kata hiyo kwenda kufanya siasa za kistaarabu katika uchaguzi wa mashina miezi michache ijayo ili waweze kupata viongozi wazuri watakaowaongoza.

“Tunatarajia kuanza kufanya chaguzi za mashina mbunge wenu anawaombeeni sana muende mkafanye uchaguzi mzuri muweze kupata uongozi utakaoongoza tene kata vizuri,msianze zile choko choko”

Katibu wa jumuiya ya wazazi wilaya ya Njombe Emmanuel Ngurukuru amewataka wanachama wa jumuiya hiyo katika kata mbalimbali kuiga mfano wa UWT kata ya Utengule ambayo imeonesha uwezo mkubwa wa kujiimarisha kiuchumi kwa kukuza mtaji mdogo walioupata kwa mwenyekiti wao wa UWT mkoa wa Njombe.

“Kwa sasa mna laki saba na elfu ishirini na tano na mheshimiwa Rais wetu anatutaka tuazimishe maazimisho ya miaka 45 kwa vitendo”alisema Ngurukuru

Shuramaid Kadaga na Lucy Mhenudzi ni baadhi ya wanachama wa jumuiya ya UWT kata ya Utengule wanasema Parachichi kwa sasa ndio zao la mkakati na lenye manufaa makubwa na kukuza uchumi wa wananchi.

Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Njombe Betreace Malekela akitoa maelekezo namna ya kupanda mche wa Parachichi wakati jumuiya hiyo ikisheherekea miaka 45 ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi katika kata ya Utengule.

Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Njombe Betreace Malekela akiongoza zoezi la upandaji wa miche ya Parachichi katika kata ya Utengule mara baada ya kutoa maelekezo namna ya kupanda Parachichi.

 

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...