Na. Damian Kunambi, Njombe

Watu 19 wanaripotiwa kuuwawa huku mabinti 57 wanaripotiwa kubakwa wilayani Ludewa mkoani Njombe katika kipindi cha mwaka mmoja wa 2021.

Akizungumza kuhusu matukio hayo mkuu wa wilaya ya Ludewa Andrea Tsere amesema katika tukio la ubakaji waathirika wakubwa ni wanafunzi wa darasa la sita hadi kidato cha nne ambapo vijana wamekuwa wakiwabaka na kuwapa ujauzito.

"Vijana wamekuwa wakikatisha ndoto za watoto wetu maana wanapobakwa wengine wanapata mimba kitu ambacho kinapelekea washindwe kuendelea na masomo hivyo natoa onyo kali kwa wote wenye tabia hiyo", Amesema Tsere.

Sanjari na hilo mkuu huyo amesema katika suala la mauaji  ya watu 19 ni katika matukio 16 ambapo baadhi ya matukio waliuwawa watu zaidi ya mmoja huku asilimia 89 za vifo hivyo vimehusishwa na imani za kishirikiana.

Hivi karibuni mkuu wa polisi wilayani humo Deogratius Masawe alipokuwa katika kikao cha baraza la madiwani alisema matukio haya yamekuwa na ugumu katika kuyafuatilia kwakuwa wahusika wa kesi hizo wengi wao wanatoa taarifa lakini wanapoitwa kutoa ushahidi hawafiki mahakamani.

Aliongeza kwa kuwaomba madiwa pamoja na vionhozi wa ngazi zote kuelimisha wananchi juu ya umuhimu wa kutoa ushahidi ili haki iweze kutendeka.
" Wanaofanyiwa vitendo vya uharifu ni wepesi kutoa taarifa lakini unapohitaji watoe ushahidi wanagoma kuja kitu ambacho kinapelekea mtuhumiwa kuonekana hana hatia na kurudi uraiani hivyo kwa hali hii matukio kama haya hayawezi kuisha" Alisema Masawe.

 Alisema " Mauaji yanayosababishwa na ushirikina mara nyingine huja kwa sababu za makusudi, mfano kuna tukio lilitokea katika kata ya Madilu wananchi walipiga kura kumtaja mchawi wa eneo hilo halafu baadae nyoka akakatiza watu wakawa wanampiga, huyohuyo aliyetuhumiwa kuwa ni mchawi akamdaka na kumuingiza ndani kwake sasa hapo sisi tufanyaje wakati ushahidi upo wazi kabisa na wananchi hawataki kuja kuutoa".

Mkuu wa wilaya ya Ludewa Andrea Tsere 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...