Na Emmanuel Massaka, Michuzi TV
BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigamboni mkoani Dar es Salaam limekutana kwenye kikao cha kawaida ambapo ajenda kuu ilikuwa kupokea taarifa za utekelezaji wa kazi katika kila Kata kwa kipindi cha robo ya pili ya Oktoba hadi Desemba.
Kikao hicho kilifunguliwa na Meya wa Manispaa hiyo Ernest Mafimbo.Pia alikuwepo Mkurugenzi, Watendaji pamoja na maofisa wengine wa idara mbalimbali.Katika mkutano huo kila Diwani amewasilisha taarifa za utekelezaji za Kata yake kisha kupitiwa na kujadiliwa na Baraza.
Wakijadili taarifa hizo za utekelezaji wa shughuli za Manispaa Madiwani wamepongeza kasi ya ulipaji wa fidia kwa kwa wananchi wa Gezaulole ambao Serikali ulichukua eneo lao kwa ajili ya upimaji viwanja
Akizungumza kuhusu suala hilo Diwani Sanya amesema kasi ya ulipaji ni nzuri, hivyo amemtaka Mkurugenzi wa Manispaa Erasto Kiwale kuendelea na kasi hiyo hatimaye kumaliza mchakato huo wa ulipaji fidia
Aidha wamepongeza jitihada za Mkurugenzi wa manispaa hiyo katika utoaji wa mikopo kwa vikundi vya vijana,wanawake na walemavu."Tumefurahishwa na kitendo cha kupewa mkopo kikundi cha Two In One kilichopo Kata ya Somangila ambacho kinachojishughulisha na shughuli za usafi, kimepewa mkopo wa Sh.milioni 55 kwa ajili ya kununua gari la kukusanya taka.
Akizungumza wakati akifunga kikao cha Baraza la Madiwani,Meya Ernest Mafimbo Ndamo amewataka watendaji kusimamia na kutekeleza maagizo na kupitia ushauri ambao umetolewa na Baraza.
Meya wa Manispaa ya Kigamboni,Ernest Mafimbo Ndamo akifungua kikao cha kawaida ambapo ajenda kuu ilikuwa kupokea taarifa za utekelezaji wa kazi katika kila Kata leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Erasto Kiwale akizungumza na madiwani wa wilaya hiyo wakati wa kikao cha kawaida ambapo ajenda kuu ilikuwa kupokea taarifa za utekelezaji wa kazi katika kila Kata leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya watumishi wa Manispaa ya Kigamboni wakimsikiliza Meya wa Manispaa ya Kigamboni,Ernest Mafimbo Ndamo.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi TV)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...