Kwa masikitiko makubwa familia ya Kubaga ya Chang’ombe Dar es salaam inawataarifu habari za kufariki kwa Mzee wetu Lay Canon Raphael Kubaga, baba mzazi wa Tino Kubaga ambaye ni Mshauri wa Walei, Mwenyekiti wa Ubaki, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji na Halmashauri ya Mtaa wa Mt. Albano.
Mipango ya mazishi inaendelea nyumbani kwake Chang’ombe TCC Club na matarajio kwa sasa ni kuwa mwili wa marehemu utapumzishwa siku ya Jumatatu.
Tutaendelea kuwaletea taarifa kadri tutakavyozipokea. Kwa sasa tuungane katika sala kuiombea faraja familia, ndugu na jamaa. Roho yake Mzee Kubaga ipate pumziko la amani milele.
- Amina.
Marehemu Mzee Kubaga alikuwa Afisa Uhamiaji Mkuu mstaafu (1969-1983) na pia Mwenyekiti wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) kwa muda mrefu.
Katika wakati wake alipokuwa Mkurugenzi wa Uhamiaji Mzee Kubaga anakumbukwa kwa mchango mkubwa katika fani ya michezo ambapo alisisitiza na kusimamia kwa umahiri michezo Idarani humo kama vile Mpira wa miguu, Mchezo wa Ngumi, Mchezo wa mpira wa Pete, Mpira wa kikapu, bila kuwasahau wanariadha mahiri kiasi hata idara ilijizolea sifa nyingi kutokana na michezo kiasi ya kwamba wanariadha na mabondia wengi wazuri walikuwa wakitokea katika idara ya Uhamiaji,nao waliweza kuwakilisha nchi nje ya nchi na kufanya vizuri.
Vijana wengi walifaidika kupitia michezo na kwa sasa wamekuwa wakitoa mchango mkubwa katika nchi hii katika maswala ya ulinzi na usalama.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...