Na John Mapepele.

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema anatarajia kukutana   na wasanii wa makundi yote katika kipindi  kifupi kijacho ili  kujua   changamoto zinazowakabili kwenye kazi zao ili kupata ufumbuzi wa pamoja.

Mhe. Mchengerwa ameyasema hayo leo Februari 3, 2022  wakati alipokutana na  kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Jacqueline Woiso katika ofisi za Wizara Mtumba jijini Dodoma.

Amefafanua kuwa ili kuleta mapinduzi katika sanaa kuna haja ya Serikali kukaa pamoja na wadau ili kujua changamoto na kuzitatua kwa pamoja.

"Nitahakikisha tunakwenda kuwanyanyua na kuboresha kazi za wasanii wetu na kuziweka katika ubora wa kimataifa kwa kushirikiana  nao ili wafaidike na kazi zao" amesisitiza Mhe. Mchengerwa.

 Aidha, ametoa wito kwa wadau wote ikiwa ni pamoja na  Multichoice Tanzania kutoa ushirikiano kwa  Serikali ili kuweza kufanikisha azma ya Serikali  ya kutoa ajira na kuboresha maisha ya wasanii hapa nchini.

Ameipongeza   Kampuni ya Multichoice Tanzania (DSTV) kwa kurusha maudhui ya kitanzania hususan Muziki na Filamu ambayo yameleta manufaa kwa wasanii.

Kwa upande wake Mkurugenzi huyo, ameahidi ushirikiano wa karibu na Wizara katika kuhakikisha sanaa inakuwa na wasanii wanapata kipato kutokana na kazi zao.

Awali, Mhe. Mchengerwa katika hotuba yake aliyoitoa kwenye  tamasha la utoaji wa tuzo za muziki na ugawaji wa mirahaba kwa wasanii alitoa wiki tatu kwa watendaji wa wizara yake kutengeneza App ya "Ongea na Waziri" ambayo ina lengo la kuwawezesha wadau wa sanaa, michezo na utamaduni kuongea moja .kwa moja na wadau hao badala ilivyokuwa awali.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...