Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro amemteua Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Michigan, Prof.Julian Murchison kuwa balozi wa hiari wa utalii wa Tanzania nchini Marekani ili kuongeza idadi ya watalii wanaotoka nchini Marekani

Hatua hiyo ni inakuja ikiwa ni jitihada za Wizara ya Maliasili na Utalii kuanza kuteka soko endelevu la Utalii la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Marekani hususan vilivyopo katika Jimbo la Michigan

Akizungumza hivi karibuni kwenye ziara ya kikazi katika mji wa Detroit nchini Marekani Waziri Ndumbaro amesema amelazimika kumteua Balozi huyo kutokana na ushawishi wake mkubwa katika jamii na pia Prof. Julian ni zao la Tanzania

Amesema Prof. Juliani amezaliwa nchini Marekani lakini amesoma na kuhitimu shahada yake ya kwanza katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na pia amekaa Tanzania kwa zaidi ya miaka 15

Aidha, Dkt. Ndumbaro amesema Prof. Julian mbali ya kuwa Mwenyeji nchini Tanzania bali ni mtu mahiri anayezungumza lugha ya kiswahili ya ufasaha wa hali ya juu.

Amesema anaamini atakuwa Balozi mzuri kwa utalii wa Tanzania kwa sababu maeneo mengi ya utalii anayajua hususani maeneo ya kusini ambako alitumia muda mwingi katika maeneo hayo kufanya utafiti.

Aidha, Dkt. Ndumbaro amuelezea Prof. Juliani kuwa ni mtu mahiri anayezungumza Lugha ya Kiswahili kwa ufasha wa hali ya juu

“ Uteuzi wake sio wa kubahatisha ni mtu ambaye amekuwa anaipenda sana nchi ya Tanzania ana amekuwa muumini mkubwa wa utalii wa utamaduni hivyo atakuwa chachu kwa Wanafunzi anaowafundisha kuwachochea kuja nchini Tanzania na hili ndo soko tunalolitaka kwa sasa'' amesisitiza Dkt, Ndumbaro


Wizara ya Maliasili na Utalii imedhamiria kukuza utalii kwa kuongeza watalii kutoka Marekani kwa kuwa nchi hiyo ni ya pili kwa kuleta watalii wengi nchini Tanzania

Kwa mujibu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, takwimu za mwaka 2020/2021 zinaonyesha Marekani ilikuwa ya tano kwa idadi ya watalii waliotembelea Tanzania huku Uingereza ikiwa ya 16.

Kwa upande wake, Prof. Julian amesema kuwa yeye atakuwa balozi mzuri katika kutangaza mazuri ya Tanzania na utalii wake duniani kote kwa wanafunzi anaowafundisha na pia kwa jamii yote inayomzunguka

“Kila nitakapopata fursa nitawaambia kuwa Tanzania ni nchi yenye watu wakarimu sana, nitazidi kuipeperusha bendera ya Tanzania na nitawaeleza sehemu mahsusi za kitalii zilizoko Tanzania.

Hata hivyo, Prof. Julian amesema hata kabla ya kuteuliwa amekuwa mstari wa mbele kutangaza vivutio vya utalii katika kazi yake anayoifanya ya kufundisha wanafunzi.


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro (wa pili kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na  Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Michigan, Prof.Julian Murchison ( wa kwanza kushoto) ambaye ameteuliwa  kuwa balozi wa hiari wa utalii wa Tanzania nchini Marekani akiwa kwenye picha ya pamoja na familia yake katika mji wa Detroit  mara baada ya kumtembelea nyumbani kwake ambaye kwa sasa anafanyia kazi nyumbani kwake kutokana na uwepo wa ugonjwa wa UVIKO -19, Wa pili kulia ni Prof. Sandra Murchison ambaye ni mke wa Prof. Juliani na kwanza kulia ni Afisa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, Jean Msabila



Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na  Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Michigan, Prof.Julian Murchison ( wa kwanza kushoto) ambaye ameteuliwa  kuwa balozi wa hiari wa utalii wa Tanzania nchini Marekani  Wa kwanza kulia ni Prof. Sandra Murchison ambaye ni mke wa Prof. Juliani




Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro (wa pili kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na  Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Michigan, Prof.Julian Murchison ( wa pili kushoto) ambaye ameteuliwa  kuwa balozi wa hiari wa utalii wa Tanzania nchini Marekani akiwa kwenye picha ya pamoja na familia yake katika mji wa Detroit  mara baada ya kumtembelea nyumbani kwake ambaye kwa sasa anafanyia kazi nyumbani kwake kutokana na uwepo wa ugonjwa wa UVIKO -19, Wa kwanza kushoto ni Prof. Sandra Murchison ambaye ni mke wa Prof. Juliani na kwanza kulia ni Afisa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, Jean Msabil

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...