Na Amiri Kilagalila,Njombe

Polisi mkoa wa Njombe wanamshikilia Israel Msigwa maarufu kwa jina la mtoa roho (39) mkazi wa Makambako kwa tuhuma za kumsababishia kifo mtoto wake Haskad Msigwa (7) kwa kumuadhibu mtoto huyo kwa nyaya za umeme na fimbo huku sababu ikitajwa ni kutokana na kukojoa kitandani.

Hayo yamebainishwa na kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Hamis Issah wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.

“Huyu amemuadhibu mtoto wake kwa kutumia waya za umeme pamoja na fimbo na matokeo yake amemsababishia kifo mtoto wake”alisema kamanda Issa

Kamanda Issa amesema mtuhumiwa huyo baada ya kutekeleza mauaji alitoweka na kukimbilia eneo la Kilosa wilaya ya Mufundi mkoani Iringa

“Mzazi huyu alitoweka na alipotoweka tumemkamata jana eneo la Kilosa Mufindi mjini Mafinga na sasa mzazi tunaye Mbaroni lakini mtoto amepoteza maisha,tukikamisha upelelezi sheria zitafuata mkondo wake”alisema Kamanda


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...