Na Amiri Kilagalila,Njombe

Baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya Njombe limepitia,kujadili na kuidhinisha mapendekezo ya mpango wa bajeti wa mwaka 2022/2023 uliofikia shilingi bilioni thelathini na moja,milioni mia tatu sabini,laki moja hamsini na mbili elfu na mia tisa themanini na tano.

Akizungumza mara baada ya kupitisha mpango huo wa bajeti,mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Njombe Valentino Hongoli amesema katika mpango huo hakuna idara ambayo imeachwa na anaamini bajeti hiyo imeweza kuzingatia malengo ya halmashauri katika kuwaletea maendeleo wananchi wa wilaya ya Njombe.

“Ninatumaini kabisa kwenye bajeti yetu inayokuja tutakwenda vizuri sana kuliko bajeti iliyopita na tutakwenda kutekeleza miradi kwenye kila maeneo vizuri”alisema Hongoli

Hongoli ametoa rai kwa watendaji kuongeza nguvu kwenye ukusanyaji wa mapato ili bajeti hiyo iweze kutekelezeka.

“Cha msingi tujikite katika kukusanya mapato kikamilifu,kwa ushirikiano kama timu kuanzia kwa mkurugenzi mpaka ngazi ya vijiji ili kuongeza ukusanyaji wa mapato”alisema Hongoli

Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya hiyo Bi.Saharifa Nabarang’anya amewashukuru madiwani kwa kupitisha mpango wa bajeti hiyo na kuahidi ushirikiano na juuhudi katika kazi ili kufikia malengo ya wananchi na halmashauri.

“Niwashukuru madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Njombe kwa kupitisha mpango wetu wa bajeti”alishukuru Bi,Nabarang’anya

Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Njombe,katibu tawala wa wilaya hiyo Emmanuel George amesisitiza kuongeza ushirikiano ili kukamilisha miradi iliyoanzishwa katika halmashauri hiyo inakamilika.

“Sisitizo letu ni kuwa miradi ile ambayo tumeianzisha tuhakikishe tunaimaliza kwa wakati ili tuweze kupata furas ya kupata fedha na kuanzisha miradi mingine,na mradi wowote unapotekelezwa katika maeneo yetu tutambue kuwa huo ni wa kwetu sote”alisema Emmanuel George.

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Njombe Valentino hongoli akitangaza madiwani wa halmashauri hiyoi kupitisha mapendekezo ya bajeti ya zaidi ya bilioni 31 kwa mwaka 2022/2023
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Njombe Bi.Sharifa Nabarang’anya wa kwanza kulia akiwa na mwenyekiti wa halamashauri hiyo pamoja na makamu mwenyekiti wakati wa baraza.

Baadhi ya madiwani wakiwa kwenye kikao cha baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya Njombe katika kikao kilicho fanyika Mtwango.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...