Baadhi ya wanafunzi wa kike wakiwa katika hafla ya shirika la REPOA ya kuadhimisha miaka 60 ya ushirikiano wao katika nyanja mbalimbali kati ya Tanzania na Marekani kwa miaka kadhaa
Afisa mahusiano na mambo ya habari kutoka katika ubalozi wa Marekani Michael Pryor,Akiwa katika Picha na katika Dr Donald Mmari ambaye ni Mkurugenzi mtendaji wa shirika la REPOA wakati hafla ya kuadhimisha miaka 60 ya ushirikiano wao katika nyanja mbalimbali kati ya Tanzania na Marekani.

Baadhi ya washiriki wa Maadhimisho 60 ya ushirikiano Kati ya Tanzania na Marekani n awakifuatilia kwa makini nada zilizokuwa zikiendelea .


Na.Vero Ignatus, Arusha.


Katika kuhakikisha wasichana wanaondokana na dhana ya kutopenda masomo ya sayansi , hesabu na uhandisi ubalozi wa marekani kwa kushirikiana na shirika la REPOA umetoa semina kwa wanafunzi wa kike kutoka katika shule mbalimbali Jijini Arusha lengo likiwa ni kuwahamasisha kujikita katika masomo hayo .

Hayo yameelezwa na Dr Donald Mmari ambaye ni Mkurugenzi mtendaji wa shirika la REPOA wakati hafla ya kuadhimisha miaka 60 ya ushirikiano wao katika nyanja mbalimbali kati ya Tanzania na marekani kwa miaka kadhaa ambapo alisema wasichana wengi wamekuwa wakikutana na changamoto mbalimbali ambazo zinawafanya kutopenda kusoma masomo hayo .

"Vijana wengi hasa wasichana wamekuwa na wakati mgumu katika kuvuka vikwazo wanavyokutana navyo katika kusoma masomo ya sayansi , hesabu pamoja na uhandisi sababu kubwa ni wanakosa ushauri mzuri , matatizo ya kifamilia na muda mwingine wazazi wamekuwa wanawakatisha tamaa katika vile vitu watoto wanavyopenda kusomea "

Sambamba na hayo pia Dr Mmari alitoa wito kwa wasichana kutosikiliza mawazo ambayo yanaweza kuwakatisha tamaa ya kutofikia malengo yao .

Naye Mwakilishi kutoka katika ubalozi wa Marekani Happy Kikwa alisema kwakuwa wanaamini katika uwezo hivyo wasichana wanatakiwa kutambua fursa ambazo zimekuwa zikitolewa kutoka sehemu mbalimbali ambazo zinahitaji watu wanaosoma masomo hayo .

"Tumekuwa tukitoa fursa mbalimbali hivyo wasichana waliopo katika nyanja mbalimbali wajue kuwa masomo ya sayansi si kwaajili ya wanaume peke yao ila wanatakiwa wapambane na masomo hayo ili waweze kupata fursa ambazo zimekuwa zikitolewa kwa watu wengi na wao wanatakiwa kuwa miongoni kwa watu wanaopata fursa hizo .

Afisa mahusiano na mambo ya habari kutoka katika ubalozi wa marekani Michael Pryor alisema katika kuhakikisha kizazi kipya katika sayansi kinaongezeka kunahitajika kuondoa vikwazo ambavyo vinafanya wanawake kukaa nyuma katika kusoma masomo ya sayansi.

Namnyaki Daniel ni miongoni mwa wanafunzi walioshiriki katika mkutano huo alisema mkutano huo umewapa fursa ya kutambua vitu vingi ambavyo anaweza akavipata kupitia masomo hayo na kuwaasa wanafunzi wa kike kujitambua na kujiamini kuwa na wao wanaweza kusoma masomo hayo na kusaidia kutengeneza kitu kinachoweza kusaidia jamii .

Februari 11 kila mwaka ni siku ya kimataifa ya wanawake na wasichana katika sayansi ambayo ilipitishwa na baraza kuu la umoja wa mataifa mnamo mwaka 2015 lengo likiwa ni kutoa fursa kwa wote katika sekta hiyo muhimu .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...