Wanawake
wamedokezwa juu ya umuhimu wa kukuza vipaji vyao vya uongozi katika
zama hizi za kampuni kubwa na kufanya kazi kwa pamoja kwa mashirika.
Hayo
yalisemwa kwenye tukio maalumu lililoandaliwa na kampuni ya SGA
Security, ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Wapendanao, ambapo
wafanyakazi wanawake ambao ni 6,000 nchini walipokea ukufunzi maalumu
juu ya uongozi na namna ya kukabili hisia kwa njia chanya.
Tukio
hilo liliwezeshwa Mzungumzaji Mtoa Motisha maarufu, George Obado,
ambaye ni mtaalamu kwenye masuala ya uongozi, na Ruth Serem, mtaalamu
katika masuala ya uwezeshaji wanawake, akiwapitisha wanawake katika
hatua mbalimbali na sifa za kile wataalamu wanachoita ‘mwanamke asiye wa
kawaida’. Kundi la wawakilishi kutoka sehemu mbalimbali za SGA
ilidokeza juu ya namna ya kukabili hisia, ikiwa ni somo la wkaati huu
kwa viongozi kwenye dunia ya leo ya kampuni kubwa kubwa.
Akizungumza
wakati wa tukio hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa SGA Tanzania, Eric Sambu,
alirejea kwamba wanawake wanahusika kwa kiasi kikubwa katika utoaji wa
uamuzi wa kimkakati. Alieleza jinsi wanawake walivyo na zawadi ya
kiasili katika kusimamia na kutatua hali mbaya na mara nyingi hufikiria
sababu zote zinazoweza kuathiri lengi na hivyo wakati mwingi huwa sawa
katika waamuayo na kufanya.
Aliwahimiza
wanawake kujiamini na kutumia faida za zawadi zao za asili kujipandisha
wnyewe kwenye nafasi za ushawishi kwenye ulimwengu huu wa ushirikiano.
Aliwasahauri dhidi ya kuwaona wenzao kuwa kana kwamba wapinzani, badala
yake wajielekeze kwenye kutwaa kinachopatikana kwenye kujuana kwao na
kufanya kazi pamoja.
Bw
George Obado alirejea juu ya haja kwa wanawake kujitambua, kudhibiti na
kuhamasishana wenyewe na kumudu vyema uhusiano, wakitazama pia wajibu
wao kijamii. Aliwashauri wawe na tunu binafsi na kumudu vyema na kiutu
uzima mihemko na ili kuganya hayo, wanatakiwa kuelewa juu ya nguvu na
udhaifu wao.
Ruth
Serem naye alitoa vidokezo juu ya jinsi ya kuwa mwanamke wa kitofauti
au asiye wa kawaida, akachukua kile alichiopata kusema Maya Abgtelou,
kwamba wamefanywa kuwa maalumu, na kwa hakika si watu wa kawaida.
Meneja
Rasilimaliwatu wa SGA Security, Bw Ebenezer Kaale, alisema kwamba
kampuni hiyo inawapa moyo wanaume katika nafasi zao kuendelea na ustawi,
akisema ndiyo siri ya mafanikio yao.
“Japokuwa
sekta ya usalama haijavuta wanawake wengi, SGA imejenga mazingira sawa
na inao wanawake wengi kwenye safu muhimu na uzoefu unaonesha kwamba
kwamba wamekuwa si wa kawaida,” alisema. “Wanawake ni waangalifu zaidi
huku wakifuata sera na kanuni zilizowekwa na kwa mara nyingi ni
waaminifu, na hizi ndizo sifa muhimu kwenye sekta hii,” akaongeza.
SGA
Security ni moja ya waajiri wakubwa zaidi nchini na kampuni kongwe
zaidi ya ulinzi, ikiwa imefanya shughuli zake tangu 1984. Hutoa huduma
maalumu katika ulinzi na usimamizi wa fedha taslimu, suluhishio kwenye
ulinzi wa kielektroniki, huduma za mwitikio wa dharura pamoja na huduma
za usafirishaji.
Baadhi
ya waajiriwa wanawake wa kamouni ya SGA Security wakisherehekea Siku ya
Wapendanao Jumatatu iliyopita. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa SGA
Tanzania, Eric Sambu na Mzungumzaji Mtoa Motisha, George Obado
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...