Na Karama Kenyunko Michuzi TV

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa taarifa ya uwepo wa kimbunga Batsirai katika maeneo ya Kusini Magharibi mwa bahari ya Hindi.

kimbunga hicho tangu ambacho kilijitokeza katika bahari ya Hindi tarehe 27/01/2022 kwa sasa kimesogea katika maeneo ya kisiwa cha Madagascar.

Katika taarifa iliyotolewa na Mamlaka hiyo leo Februari 4,2022 imesema uchambuzi wa mifumo ya hali ya hewa unaonesha kutokuwepo kwa uwezekano wa kimbunga hicho cha Batsirai kufika katika Pwani ya Tanzania lakini uwepo wake baharini unatarajiwa kuathiri mifumo ya hali ya hewa kwa baadhi ya maeneo hapa nchini ikiwa ni pamoja na kusababisha ongezeko la mvua; vipindi vya upepo mkali unaofika na kuzidi km 40 kwa saa na mawimbi makubwa baharini yanayozidi mita 2 hasa kwa maeneo ya ukanda wa pwani.

Taarifa hiyo pia imeyataja maeneo yanayotarajiwa kupata vipindi vya mvua kubwa kutokana na uwepo wa kimbunga hicho baharini kati ya tarehe 04 hadi 08/02/2022 ni pamoja na mikoa ya Mtwara, Lindi, Ruvuma, Morogoro, Pwani, Singida, Dodoma, Iringa, Njombe, Mbeya, Songwe na Rukwa.

Hata hivyo mvua za Msimu zinaendelea katika maeneo mengine yanayopata mvua hizo.

Hata hivyo wakati, Mamlaka inaendelea kufuatilia mwenendo wa kimbunga hicho, inawashauri wananchi kuendelea kufuatilia na kuzingatia taarifa za utabiri kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania pamoja na kupata ushauri na
miongozo ya wataalam katika sekta husika ili kupunguza athari zinazoweza kujitokeza.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...