NA
K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, MOROGORO.
KATIBU
Mkuu wa TUGHE taifa Bw. Hery Mkunda amepongeza Uhusiano mzuri baina ya
Menejimenti ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) na Wafanyakazi .
Bw.
Mkunda ameyasema hayo mjini Morogoro Februari 11, 2022 wakati wa kikao cha
Baraza la Wafanyakazi la WCF.
“Baraza
la Wafanyakazi ni chombo cha ushauri kwa Menejimenti na kinawakilisha
wafanyakazi kutoka idara na mikoa , nimeona kuna ushirikishwaji mkubwa kwenye
taasisi hii ukilinganisha na taasisi nyingine, naomba niwapongeze sana.”
Alisema Bw. Mkunda
Aliwakumbusha
wafanyakazi wajibu wao kwa mwajiri “Kudai maslahi ni jambo moja lakini pia lazima
wafanyakazi watambue kuwa wanao wajibu wa kwenda kufanya kwa mwajiri ili
kuhakikisha yale maslahi ambayo wafanyakazi wanadai yawe na uhalali.”
Alifafanua.
Awali
Mwenyekiti wa TUGHE tawi la Mfuko wa
Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bi. Amina Likungwala aliupongeza Uongozi wa Mfuko kwa mahusiano mazuri na
Wafanyakazi.
"Napenda
kuipongeza Menejimenti ya WCF kwa mahusiano mazuri na Wafanyakazi, na
ushirikiano ndani ya Baraza hili, kwakweli tunapata ushirikiano wa kutosha na
tunajadiliana kwa uwazi" Alisema.
Alisema
hoja za wafanyakazi zilizopelekwa kwenye Menejimenti kwa kiasi kikubwa
zimefanyiwa kazi na TUGHE ina imani hata zile hoja zilizosalia nazo zitafanyiwa
kazi.
Aidha,
Katibu wa TUGHE mkoa wa Dar es Salaam, Bi. Sara Rwezaura aliwahimiza
wafanyakazi ambao hawajajiunga na TUGHE wafanye hivyo kwani ni chombo muhimu
kwa wafanyakazi.
Akifunga
kikao hicho, Mwenyekiti wa Baraza ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa
Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. John Mduma
alisema maamuzi yanayopitishwa ndani ya Baraza ni kwa ajili ya maslahi ya Taasisi na ndio maana baraza hili
lina umuhimu mkubwa.
“Sisi
tumekuja hapa kwa uwakilishi, tuendelee kuwahamasisha wenzetu kwa kuwapa
mrejesho kutokana na maamuzi tuliyofikia.” Alisema.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...