Waandaaji
wa mbio maarufu za Kilimanjaro Premium Lager Marathon 2020 wamesema
kuwa licha ya usajili wa mbio za Km 42 na Km 21 kufungwa baada ya kujaa,
usajli wa mbio za Km 5 bado unaendelea kwa njia ya Tigo Pesa.
Taarifa
iliyotolewa Jijini Dar es Salaam ilisema kuwa usajili wa mbio za Km 42
na 21 ulifungwa tangu Februari 7, 2021 baada nafasi zote kujaa.
“Tumefunga
kabisa usajili wa mbio hizo mbili lakini usajili wa Km 5 unaendelea kwa
njia ya Tigo Pesa kwa kubonyeza *149*20#. Hii ni njia nyepesi ya
kujisajili na tunatoa wito kwa washiriki wote wajisajili mapema kuepuka
usumbufu dakika za mwisho,” walisema waandaaji hao.
Usajili
huu pia utafanyika wakati wa zoezi la uchukuaji namba za kukimbilia
Jijini Dar es Salaam, Arusha na Moshi. Hata hivyo tunatoa wito kwa
washiriki wote wajisajili kwa njia ya simu kuepusha usumbufu,” ilisema
taarifa hiyo.
Wadhamini wa mbio za Kilimanjaro Marathon 2022 ni Kilimanjaro Premium Lager (Mdhamini Mkuu) Tigo (21km) na Grand Malt (5km).
Wadhamini
wa meza za maji ni pamoja na Absa Tanzania, Unilever Tanzania, TPC
Sugar, Simba Cement na Kilimanjaro Water. Wasambazaji rasmi ni
GardaWorld Security, Keys Hotel, Kibo Palace Hotel, CMC Automobiles na
Surveyed Plots Company Ltd (SPC) na Bodi ya Utalii (TTB).
Katika
hatua nyingine, maandalizi ya maonesho yanayojulikana kama Kili Expo
(The People's Expo) ambapo wadhamini na wadau wengine wa mbio hizo
watapata fursa ya siku tatu za kuonyesha bidhaa na huduma wanazotoa
yamekamilika.
Maonyesho hayo yanatarajiwa kufanyika kati ya Februari 24-26, 2022, katika viwanja vya MoCU na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali.
"Maonyesho
haya pia linakusudiwa kuwapa uma uzoefu wa muda mrefu wa mbio za Kili
Marathon; pia kwa mwaka huu wanaotarajia kushiriki mbio hizo watapata
fursa ya kuchukua namba zao za ushiriki eneo la chuo kikuu cha Ushirika
badala ya eneo la Keys Hotel kama ilivyokuwa miaka ya nyuma”, ilisema
taarifa hiyo ya wandaaji.
Mbio
za Kilimanjaro Premium Lager Marathon, zinatarajiwa kufanyika Jumapili
ya Februari 27, 2022, katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi
(MoCU), ambapo zimeandaliwa na taasisi ya Kilimanjaro Company Limited na
kuratibiwa na wadau wa hapa nchini kampuni ya Executive Solutions
Limited
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...