Na Jonas Kamaleki, Mbeya
Serikali imewaasa wanahabari kuibua fursa za kiuchumi zilizopo Nyanda za Juu Kusini na sehemu nyinginezo nchini Tanzania ili kuwafanya wananchi na wawekezaji wa ndani na nje kuzitumia kwa ustawi wao na Taifa kwa ujumla.
Hayo yamesemwa leo jijini Mbeya na Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (Usimamizi wa Sekta ya Fedha), Dkt. Bernard Kibesse wakati akifungua Semina ya Benki Kuu kwa Waandishi wa Habari za Biashara, Uchumi na Fedha.
Akitoa hotuba kwa niaba ya Naibu Gavana, Kaimu Mkurugenzi wa Tawi la Benki Kuu Mbeya, Dkt. Nicholaus Kessy amesema Mkoa wa Mbeya na mikoa mingine ya Nyanda za Juu Kusini yaani Songwe, Njombe, Katavi na Iringa ina fursa nyingi za kiuchumi ambazo hazijatumika ipasavyo ili kuchangia katika uchumi wa nchi.
“Fursa hizo ni pamoja na ardhi nzuri ifaayo kwa uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara, hali ya hewa nzuri pamoja na vivutio vingi vya utalii”amesema Dkt. Kessy na kuongeza kuwa waandishi wa habari pamoja na vyombo vyenu mna nafasi ya kuziibua fursa hizo kwa kuzitangaza na kuvutia watalii kufika katika mikoa hii na kuchangia maendeleo ya nchi yetu.
Ametaja vivutio hivyo kuwa ni pamoja na Mbuga za Taifa za Kitulo, Ruaha na Katavi na kuongeza kuwa hazipati wageni wengi kwani hazitangazwi sana hivyo kuwaomba wanahabari kuzitangaza kwa nguvu zote.
“Mkidhamiria kubadilisha hali hii mnaweza kuifanya Kanda hii iwe maarufu kama ilivyo Kanda ya Kaskazini kwa masuala ya utalii’, alisisitiza Dkt. Kessy.
Akizungumzia mchango wa vyombo vya habari kuhusu kutangaza habari za biashara, uchumi na fedha, Dkt. Kessy alisema kuwa Benki Kuu ya Tanzania inatambua na kuthamini kazi kubwa inayofanywa na vyombo hivyo katika maendeleo ya Taifa.
Mada zitakazotolewa ni pamoja na Viwango vya Ubadilishanaji Fedha, Biashara katika Soko la Hisa la Dar es Salaam, Minada ya Dhamana za Serikali na nyingine nyingi zinazohusu masuala ya Fedha. Semina hii inahusisha washiriki Zaidi ya 43 toka vyombo vya habari vya umma na binafsi na imeandaliwa na Benki Kuu ya Tanzania.
Kwa Zaidi ya miaka minane, Benki Kuu imekuwa ikiendesha semina kwa waandishi wa habari angalau mara moja kwa mwaka ili waweze kuielewa Benki hiyo na kupitia uelewa wao huo waweze kuelimisha umma kuhusu kazi za Benki Kuu na masuala ya Fedha, Biashara na Uchumi kwa ujumla.
Meneja Uchumi Tawi la Benki Kuu Tanzania- Mbeya Dkt Nicholaus Kessy akifafanua kuhusu Malengo ya Sera ya Fedha ya Mwaka 2021/22 katika soko huria mbele ya Wandishi wa Habari kutoka Tanzania Bara na Visiwani wanaoshiriki Semina ya tisa ya Waandishi wa habari za Uchumi ,biashara na fedha inayofanyika katika tawi la BoT Mkoani Mbeya.
Lengo la Semina hiyo ya siku tano ni kuongeza uelewa wa Waandishi wa Habari kuhusu majukumu ya Msingi ya @bankoftanzania,kukuza umahiri katika uandishi wa habari za Uchumi, Biashara, Fedha na pia kuimarisha ushirikiano baina ya BoT na Waandishi wa Habari.
Meneja Uchumi Tawi la Benki Kuu Tanzania- Mbeya Dkt Nicholaus Kessy akifafanua jambo mbele ya Wandishi wa Habari kutoka Tanzania Bara na Visiwani wanaoshiriki Semina ya tisa ya Waandishi wa habari za Uchumi ,biashara na fedha inayofanyika katika tawi la BoT Mkoani Mbeya.
Meneja Uchumi Tawi la Benki Kuu Tanzania- Mbeya Dkt Nicholaus Kessy akiwasilisha mada iliyohusu namna Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inavyoaandaa na kutekeleza sera za fedha mbele ya Wandishi wa Habari kutoka Tanzania Bara na Visiwani wanaoshiriki Semina ya tisa ya Waandishi wa habari za Uchumi ,biashara na fedha inayofanyika katika tawi la BoT Mkoani Mbeya.
Lengo la Semina hiyo ya siku tano ni kuongeza uelewa wa Waandishi wa Habari kuhusu majukumu ya Msingi ya Benki Kuu ya Tanzania,kukuza umahiri katika uandishi wa habari za Uchumi, Biashara, Fedha na pia kuimarisha ushirikiano baina ya BoT na Waandishi wa Habari.
Kaimu Meneja Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki, Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bi. Vicky Msina akito maelekezo kwa Washiriki wa Semina hiyo namna itakavyoendeshwa wakiwemo na Watoa Mada wataalamu kutoka BoT.
Afisa Uhusiano Mkuu wa Benki kuu ya Tanzania Lwaga Mwambande akifurahia jambo na Mwandishi mkongwe Laudeni Mwambona kabla ya kufunguliwa rasmi kwa Semina ya Waandishi wa habari inayofanyika jijini Mbeya,kulia ni Mwanahabari Mwandamizi kutoka K-Vis Blog, Khalfan Said . PICHA ZOTE NA MICHUZIJR-MICHUZI MEDIA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...