Uzinduzi wa huduma kwenye ofisi mpya za Tanesco mkoa wa Kagera ukiongozwa na Afisa Mkuu wa fedha Tanesco (CFO) CPA. Renata Ndege akikata utepe kuashiria kuzinduliwa rasmi kwa hutoaji huduma
12/02/2022
Na Samuel Mandari
AFISA UHUSIANO - TANESCO KAGERA.
TANESCO MKOA wa Kagera imezundua rasmi utoaji wa Huduma kwenye ofisi mpya za mkoa zilizopo Bukoba Manispaa mtaa wa Jamhuri Mkabala na kanisa la Roman Catholic Cathedral.
Akizungumza Wakati wa uzinduzi huo wa kuanza kwa huduma, CFO wa Tanesco Bi Renata Ndege ambaye aliambatana na Viongozi mbalimbali, Meneja wa Kanda ya Ziwa Eng. Henryfrid Byabato, Meneja wa Mkoa Kagera Eng.Godlove Mathayo, Grace Ndibalema - Afisa Miliki Mkuu, amewakaribisha rasmi wateja na wakazi wa mkoa wa Kagera kupata Huduma Kupitia ofisi hizo. "TANESCO tunaendelea kuboresha Huduma zetu na Safari hii tumefanikiwa kujenga Jengo hili ili kurahisisha Huduma kwa Wateja wa Mkoa wa Kagera, ofisi zetu zimejengwa katika mpangilio mzuri sana utakaowezesha Wateja wetu kupata Huduma katika utaratibu rahisi wa Huduma zote Ndani ya Duka Moja (one stop shop) Sasa Tunawakaribisha wateja na wananchi Wote kupata Huduma Bora Ndani ya ofisi hizi"
Tukio Hilo la ufunguzi liliambatana na Tukio la Viongozi, Wafanyakazi na wateja kukata na kula pamoja keki ya upendo iliyobeba ujumbe elekezi wa CORE VALUE za Shirika Customer first, Safety, Integrity,Team work, Innovation, Passion.
Mmoja Kati ya Wateja waliohudhuria uzinduzi huo Ndugu Deus Majura amewapongeza TANESCO kwa kufungua ofisi ya kisasa na uboreshaji wanaondelea kufanya Ndani ya Mkoa.
Meneja wa Mkoa Mhandisi G.Mathayo akiwakaribisha Wateja ofisini hapo na kuwahakikishia upatikanaji wa Huduma Bora pia alitumia nafasi hiyo kuwajulisha Wateja waliolipa siku za nyuma watapata Huduma ya Umeme Kabla ya 31/03/2022
Kabla ya tukio hili la Uzinduzi Kulitanguliwa na Bonanza la Michezo iliyowashirikisha Wafanyakazi wa Wilaya Zote za mkoa wa Kagera na Baada ya uzinduzi huo ilifuata Sherehe ya usiku iliyofanyika Ukumbi wa Eco Beach Club na Kuhudhuriwa na Naibu Waziri Nishati Wakili Stephen Byabato ambae katika salamu zake aliwataka Wafanyakazi kufanya Kazi kwa bidii na kuwahakikishia wizara iko pamoja nao kuhakikisha wanafikia malengo waliyojiwekea.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...