Na Said Mwishehe,Michuzi TV 

WAKALA wa Usajili wa Biahara na Leseni (BRELA) umesema katika kipindi cha siku tano za mwanzo ambazo wamekuwa wakitoa elimu kuhusu umuhimu wa wananchi kusajili biashara zao pamoja na kutoa huduma mbalimbali wananchi 1000 wamehudumiwa.

Katika siku hizo BRELA imekuwa ikiwahudumia wananchi katika viwanja vya Mliman City mkoani Dar es Salaam na baada ya kuonekana idadi imekuwa kubwa Mtendaji Mkuu wa Wakala huo kwa mamlaka aliyonayo ameongeza siku nyingine tatu, hivyo watakuwepo hapo hadi Jumatano ya wiki hii.

Akizungumza na Michuzi Blog, Ofisa Leseni BRELA Robert Mashika, amesema zipo sababu kadhaa za kuwafanya watoke ofisini na kuwafuata wananchi kwenye eneo hilo na moja sababu ni baaa ya kuona malalamiko kuna mengi kuhusu huduma za usajili.

"Pia ni kawaida ya BRELA kila mwaka kutoka ofisini na kuwafuata wananchi ili kuwapa elimu ya umuhimu wa kusajili biashara zao na wakati huo huo kuwahudumia , ndio maana tumekuwa tukishiriki kwenye maonesho kadhaa, kwa mfano Sabasaba, Nane Nane, Wiki ya Dhahabu Geita na mara nyingi BRELA inaandaa mabanda yake na kutoa elimu na huduma mbalimbali.

"Kwa mwaka huu moja ya mkakati wetu tutakwenda kila mkoa, kila wilaya ilimradi kila mtu awe na elimu ya usajili , tunavyoenda huko mbele biashara zote zitatakiwa kusajiliwa , hivyo watu wasije kusema wamekosa usajili ,kila aina ya biashara inatakiwa kusajiliwe.

"Hata hata biashara zinazofanyika Online zinatakiwa kusajiliwa ,na wengi ambao wamefika kuhudumiwa ni wale wanaofanya biashara kwa njia ya online,"amesema Mashika.

Kuhusu siku tano za mwanzo ambazo wamehudumia wananchi, amesema wengi wao wamesajili majina ya biashara, wengine wamesajili kampuni, kupata leseni na huduma nyingine, na kwa siku walikuwa wakihudumia watu kati ya 150 hadi watu 200, hivyo watu waliohudumiwa ni 1000 na wanaamini baada ya kuongezwa tena siku nyingine tatu idadi itaongezeka zaidi.

Aidha amesema wamebaini wateja wengi sio wameshindwa kufanya sajili lakini hawafahamu jinsi ya kujaza domu mtandaoni."Mteja anakuja kulalamika amefanya maombi muda mrefu lakini ukienda kwenye akaunti yake unakuta siku aliyofanya maombi ndio siku aliyojibiwa au alishapata mpaka usajili.

"Kwa kutojua mfumo unakuta mtu analalamika , tumekuta hakuna sababu ya msingi ya watu kutomaliza sajili zao, unakuta mwingine ameshindwa kuandika sehemu anayoishi , au aina ya biashara anayotaka kuifanya, na wengine hawakujaza chochote.Hivyo tunayo timu ya maofisa wasaidizi ambao wamekuwa wakisadia kuweka kila kitu sawa,"amesema Mashika.

Amefafanua shughuli nyingi za BRELA ziko kwenye mfumo, hivyo ni ngumu kukwepa mfumo huo lakini  kupitia elimu wanayotoa kwa wananchi wanaamini itasaidia kuondoa baadhi ya changamoto.

Alipoulizwa ni vitu gani ambavyo anayetaka kusajili biashara yake au kampuni anatakiwa kuwa navyo, amesema kitambulisho cha Taifa (NIDA) ni muhimu kuwa nacho maana ndio kama funguo ya kuingia katika mfumo wa kusajili , lakini pia kwa wale wanaotaka kusajili kampuni lazima wawe na makubaliano ambayo yametengenezwa na wanasheria."Mtu anayesajili jina la biashara akiwa na kitambulisho cha NITA tu inatosha."





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...