Mhe. Mchengerwa akiongea na umati wa wageni walioshiriki kwenye kilele cha Tamasha la Sauti za Busara Februari 13, 2022 ZanzibarWaziri
Mchengerwa akiteta jambo na Katibu Mkuu wake Dkt.Hassan Abbasi mara
baada ya kuwasili kwenye kilele cha Tamasha la Sauti za Busara, huko
Zanzibar Februari 13, 2022.
Umati wa watu waliohudhuria kwenye kilele cha tamasha la Sauti za Busara Februari 13, 2022 huko Zanzibar.
Mhe.
Mchengerwa akitambulishwa na kamati ya maandali ya tamasha la Sauti za
Busara ili aongee na umati wa watu walioshiriki kwenye kilele cha
tamasha hilo usiku wa kuamkia leo Februari 14, 2022 Zanzibar
Wasanii mbalimbali wakitumbuiza kwenye kilele cha tamasha la Sauti za Busara huko Zanzibar, Februari 13, 2022
**************************
Na. John Mapepele
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa amewakaribisha wageni mbalimbali waliohudhuria tamasha kubwa la kimataifa la Sauti za Busara kutoka sehemu mbalimbali duniani kushiriki kwenye tamasha la kihistoria la muziki la Serengeti litakali fikia kilele chake Machi 12, mwaka huu jijini Dodoma.
Akizungumza kwenye kilele cha Tamasha la Sauti za Busara usiku wa kuamkia leo Februari 14, 2022 huko zanzibar amesema Serikali inakwenda kuandaa matamasha makubwa ya kihistoria ambayo yataonesha utamaduni wa kitanzania, hivyo dunia inakaribishwa kushuhudia tukio hili la kihistoria na kimataifa.
“Naomba kutumia nafasi hii kuwakaribisha kwenye Tamasha la Serengeti na Tamasha la kimataifa la Sanaa na Utamaduni la Bagamoyo ambayo yanakwenda kuionyesha dunia utajiri wa utamaduni na vivutio vya utalii duniani”. Ameongeza Mhe. Mchengerwa.
Mhe. Mchengerwa pia aliambatana na Katibu Mkuu wake, Dkt. Hassan Abbasi na Mkurugenzi wa Sanaa . Dkt. Emmanuel Ishengoma.
Amepongeza Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo kwa kuandaa Tamasha hilo kwa kiwango cha kimataifa na kusisitiza kuwa Serikali itashirikiana nao ili kuhakikisha tamasha lijalo linafanyika.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...