Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Nchi ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Mhe.Sheikh Abdullah bin Zayed Al Nahyan tarehe 13 Februari, 2022 ametembelea Banda la Tanzania kwenye Maonesho ya Expo 2020 Dubai na kupokelewa na Balozi wa Tanzania wa Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu (UAE) Mhe.Balozi Mohamed Abdullah Mtonga ambaye pia ni Kamishna Jenerali wa Banda la Tanzania kwenye Maonesho ya Expo 2020 Dubai.

Mara alipowasili kwenye Banda la Tanzania, Mheshimiwa Balozi alitumia fursa hiyo kumshukuru Mgeni wake Mhe. Zayed kwa kuchagua kuitambelea Tanzania miongoni mwa nchi washiriki 192. Aidha, aliishukuru Serikali ya UAE kwa kuandaa vizuri Maonesho makubwa ya Expo 2020 Dubai Pamoja na uwepo wa changamoto ya kuenea kwa ugonjwa wa COVID -19. Katika Maonesho haya Tanzania ni miongoni mwa nchi 50 ambapo kwa mara ya kwanza zinashiriki kwenye mabanda la pekee yaliyojengwa kwa ufadhili wa Serikali ya UAE

Mwisho Mhe. Zayed aliipongeza Tanzania kwa kuwa na Banda lenye mvuto na linaloinyesha vivutio vya utalii pamoja na fursa zilizoko katika sekta mbalimbali. Ushiriki huu wa nchi unaoratibiwa na TanTrade unatarajiwa kuwa na matokeo yenye tija na kuongeza idadi ya Watalii watakaoiembelea Tanzania, kupatikana kwa wawekezaji, mitaji pamoja na masoko ya bidhaa zinazozalishwa nchini Tanzania.

Tarehe 26 Februari, 2022 Tanzania itasherekea Siku ya Kitaifa (National Day) ambapo itafuatiwa na Kongamano kubwa la Biashara na Uwekezaji litakalofanyika tarehe 27 Februari, 2022 katika Ukumbi wa Ballon, Hoteli ya Jumeirah Beach, Dubai. Maonesho ya Expo 2020 Dubai yalianza rasmi tarehe 01 Oktoba, 2022 na yatafungwa rasmi tarehe 31 Machi, 2022. 

 




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...