Na Khadija Kalili
MKUU wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakar Kunenge amezindua Kituo Cha uwezeshaji wa huduma za wawekezaji kituo cha pamoja (One Stop Center).
RC Kunenge alisema kuwa Kitengo hicho kinajumuisha Watendaji kutoka Wizara na Taasisi mbalimbali kwa ajili ya kurahisisha mchakato wa wawekezaji kupata leseni za uwekezaji ndani ya Mkoa wa Pwani kwa haraka.
"Lengo ni kuhakikisha wanatoa huduma nzuri kwa wawekezaji Pwani ili kuwarahisishia kupata fursa mbalimbali ndani ya Mkoa" alisema Kunenge.
"Jambo hili litaweza kutoa taarifa kwa wadau wa ndani na nje ya Mkoa wetu kwamba una fanya nini na fursa zake zilizomo kuweza kutangazika kwa ujumla alisema.
"Uzinduzi wa Kituo hiki ni agizo la Rais wa awamu ya Sita Mama Samia Suluhu Hassan kama alivyoagiza vituo hivi vianzishwe nchi nzima hivyo na sisi Pwani tumetekeleza" alisema RC Kunenge.
Hivi Sasa tumeshawaandiki EPZA pindi wanapopata mwekezaji lazima taarifa za muhusika zipite ndani ya kituo hiki.
Awali akizungumza kabla ya uzinduzi huo Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani (RAS) Mhandisi Hajat Mwanasha Tumbo alisema kuwa sababu zilizopelekea kuanzishwa kwa kituo hiki ni kwa sababu wawekezaji wamekua wakifanya biashara zao bila kujitangaza ipasavyo hivyo baada ya kugundua hilo kuanzia Sasa itabidi wafuate utaratibu wa kufahamika ndani ya Mkoa wa Pwani kwa sababu awali wawekezaji hai walikua walienda EPZA moja kwa moja na baada ya hapo huenda kwenye maeneo ya uwekezaji bila ya Mkoa kuwatambua, tayari tumewaandikia barua EPZA kuwa kuwanzia sasa wakimpitisha mwekezaji yoyote bila kumpitisha Pwani hatutamtambua hivyo wazingatie utaratibu huu.
Uzinduzi wa kituo hicho umefanyika leo asubuhi, katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Pwani zilizopo Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani.
Baadhi ya Taasisi hizo wezeshi zitakazokuwa zikipatikana ni pamoja na Idara ya Uhamiaji, Brela, RUWASA, TANESCO, Zimamoto, Utumishi,DAWASCO.TRA, NEMC.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...