Na John Walter-Manyara


Kijana mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Said, ameuawa kwa kushambuliwa na wananchi wenye hasira kali baada ya kudaiwa kumuua mpenzi wake aliyefahamika kwa jina la Rukia (17-19) mkazi wa kitongoji cha Mbugani kijiji cha Magugu wilayani Babati mkoani Manyara kwa kumchinja huku ikidaiwa sababu ni wivu wa Mapenzi.


Baadhi ya Mashuhuda wa tukio hilo wameeleza kuwa wamesikitishwa na tukio hilo kwa kuwa binti huyo alikuwa bado mdogo.


Diwani wa kata ya Magugu Filbert Modamba amethibitisha kutokea kwa tukio ambapo amesema chanzo ni ni wivu wa kimapenzi uliotokana na msichana huyo ambaye kwa sasa ni marehemu kuwa na mahusiano na mwanaume mwingine baada ya mpenzi wake wa awali kuwa amesafiri kwa muda mrefu ndipo aliporudi na kumkuta binti huyo na mwanaume mwingine.


Modamba amesema baada ya tukio hilo, mtuhumiwa alitoroka ambapo jitihada za kumtafuta zilifanyika na jumatatu Machi 14 wananchi wenye hasira kali walimpata na kumshambulia hadi kifo chake.


Mwenyekiti wa kijiji cha Magugu Deogras Ngalawa amesema binti huyo ameuawa kwa kuchinjwa na kitu chenye ncha kali machi 13,2022 saa tatu usiku.


 

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...