Na Said Mwishehe, Michuzi TV

UBALOZI wa Ufaransa nchini Tanzania umesaini makubaliano mapya na Bodi ya Shule ya kimataifa ya Kifaransa ya Arthur Rimbaud ikiwa ni mkakati wa kuboresha utoaji wa elimu bora.

Akizungumza leo Machi 14,2022, Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Nabil Hajlaoui amesema makubaliano hayo yamekusudia kuboresha mazingira thabiti ya elimu kupitia shule hiyo hasa kwa kutambua siku za hivi karibu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alifanya ziara nchini Ufaransa na miongoni mwa mambo yaliyozungumwa kwa kina ni namna ya nchi hizo kusaidiana kuboresha sekta hiyo

"Makubaliano haya kati ni kati ya shule na Wakala yanayokusudia utolewaji wa elimu rasmi chini ya Wizara ya Elimu nchini Ufaransa na usimamizi wa ubalozi wa ufaransa hapa nchini , kupitia mtandao wa shule za kifaransa, kwa wanafunzi wanaosama katika shule hii ambao ni Watanzania wanaweza kunuifaka na mjumuiko wa wanafunzi wengine kutoka mabara matano,"amesema Balozi Hajlaoui.

Aidha amesema makubalo kati ya Ufaransa na shule hiyo yaliingiwa kwa mara ya kwanza mwaka 1967 ikiwa ni madhubuti wa ushirikiano baina ya nchi yao na Tanzania katika kuendelea elimu na utamaduni."Shule ya Ufaransa imeendelea kukua na kufikia idadi ya wanafunzi 400 kutoka mataifa mbalimbali, ikijumuisha theluthi tatu ya watoto wa kitanzania kwa ngazi ya awali hadi sekondari.Hivyo makubaliano ya leo ni muhimu kwa pande zote".

Amefafanua shule hiyo inawawezesha wanafunzi kuwa na uelewa wa lugha mbalimbali ikiwemo Kingereza, Kifaransa na Kihispaniola.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Ufaransa Rajab Katunda amesema shule hiyo ilianzishwa mwaka 1967 na hiyo ilitokana na ushirikiano kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Ufaransa.

Amefafanua kuwa walifanya makubaliano ya kubadilishana tamaduni na elimu zaidi."Kupitia makubaliano yaliyoingiwa huko awali Ufaransa imeendelea kusaidiana na Tanzania katika kutatua changamoto mbalimbali za kielimu shuleni kwetu."

"Kupitia makubaliano haya kuna baadhi ya vipengele , mikataba na vibali ambavyo Serikali yetu ya Tanzania inatoa katika kudumisha ushirikiano huu, shule yetu hadi leo hii tuna asilimia 30 watanzaia wanaolipa ada na wengine wanasoma kwa mkopo na asilimia iliyobaki imegawanywa kwa wafaransa na mataifa mengine yaliyobakia karibia asilimia 40 ambayo yapo kwenye shule yetu."

Aidha amesema katika kuunga mkono juhudi za Serikali ya Tanzania katika sekta ya elimu, taasisi ya shule hiyo wanashirikiana na Ubalozi wa Ufaransa kuboresha sekta hiyo.
Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Nabil Hajlaoui(wa nne kushoto) akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Kimataifa ya Kifaransa Rajab Katundu(wa nne kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa shule hiyo pamoja na maofisa wa ubalozi baada ya kusainiwa kwa makubaliano mapya ya kutoa elimu bora.Makubaliano hayo yamesainiwa leo Machi 14,2022.
Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Nabil Hajlaoui (kushoto)akisani makubaliano ya utoaji elimu bora katika Shule ya Kimataifa ya Kifaransa iliyopo Masaki jijini Dar es Salaam.


Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Shule ya Ufaransa wakiwa katika makini kufuatilia maelezo yaliyokuwa yakitolewa kabla ya kusainiwa kwa makubaliano mapya kati ya Ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania na Badi ya Shule hiyo.

Mwenyekiti wa Bodi wa Shule ya Kifaransa Rajabu Katundu akizungumza kabla ya kusainiwa kwa makubaliano hayo katika makazi ya Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania.

Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Ufaransa Diana Neivasha(kulia) akifafanua jambo kuhusu shule hiyo baada ya kusainiwa kwa makubaliano hayo.

Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Nabil Hajlaoui(katikati) akisisitiza jambo kwa wajumbe wa Bodi ya Shule ya Ufaransa kabla ya kusainiwa kwa makubaliano mapya yaliyolenga kuboresha utoaji elimu bora.

Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Nabil Hajlaoui(kulia) akielezea mikakati ya Serikali ya Ufaransa katika kusaidiana na Serikali ya Tanzania kushirikiana kuboresha sekta ya elimu nchini kupitia Shule ya Ufaransa ambapo asilimia 30 ya wanaosoma shuleni hapo ni Watoto wa Kushoto ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Calorine Damass


Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Ufaransa Rajab Katundu akijiandaa kusaini makubaliano kati ya shule hiyo na Ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania.Makubaliano hayo yanalenga utolewaji wa elimu bora



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...