Na.Vero Ignatus Arusha.

 Ilikomesha vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto ni muhimu kuwawezesha wanawake ili kujikwamua  kiuchumi na kijamii,kwani asilimia 3% ya pato la taifa hupotea kwasababu ya kushughulikia masuala ambayo yanaletwa na unyanyasaji wa kijinsia

Hayo yamesemwa na mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela  katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani 8machi 2022 mkoani Arusha, katika uwanja wa kumbukumbu wa shekh Ameri Abeid kwamba ukatili utakapokomeshwa itasaidia kuokoa rasilimali fedha nyingi zinazopotezwa kutokana na athari za unyanyasaji na kutokuwa na usawa wa kijinsia.

’Mimi naamini wanaume wenzangu sasahivi tunajihisia Amani na rah asana kuliko tunavyodhaniwa maana yake kuna wakati wanadhani wanaume tunawasiwasi sasahivi ndio tuna amani nafuraha kubwa zaidi kwasababu tuanajua jamii yetu ilivyo,wakina mama hawa wakienda mbele wakawa na nguvu zaidi hata sisi maendeleo hayo yatatugusa

Naibu Waziri wa Katiba na sheria Mhe.Geofrey Pinda Amesema kuwa kamati hizo zikisimamiwa kama inavyotakiwa itapunguza ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwani   umiliki wa ardhi umekuwa ni kizungumkuti kwa wakinamama kwani hawapewi nafasi saw ana baba hivyo wizara inaendelea kuliangalia sualahilo

Pinda amesema kuwa Maadhimisho ya  siku ya mwanamke duniani ninkutathimini na kuheshimu mchango wa mwanamke duniani katika nyanja zote za uchumi kiutamaduni,kisiasa kijamii katika kuleta Maendeleo katikabya kweli ukizingatia kuwa katika tamaduni.

 Pinda amesema kuwa katika mizunguko ambayo amekuwa nikiiifanya kuzungukia mikoa  kuwasikiliza wananchi matatizo ya wananchi mengi kati yao yamekuwa suala la ndoa,mirathi na migogoro ya ardhi  hivyo serikali inaendelea kulifanyia kazi katika kulichakata.

Lipo tatizo la mirathi ,watoto na wajane haswa wakina mama na watoto, amekuwa wakipata matatizo na migogoro mingi, Wizara ina ndelea kuangalia suala hili,marekebisho ya sheria ya ndoa haswa Binti anatakiwa aolewe akiwa na umri gani,tunaendelea na mchakato pamoja na utafsiri wa sheria.Alisema Mhe.Pinda

 Kwa upande wake Naibu katibu mkuu wa wa wizara ya maendeleo ya jamii jinsia ,wanawake na watu wenye mahitaji maalum Amon mpanju ameiomba mikoa kuhakikisha kuwa inaanzisha na kusimamia kamati za ulinzi wa wanawake na watoto yaani MTAKUWA ili jamii jamii iweze kushiriki katika kupambana na vitendo vya ukatili nchini .

Akisoma risala kwa niaba ya Wanawake kwa mgeni rasmi  Upendo Laboya alisema madhumuni ya siku hiyo ya Wanawake kujenga ushirikiano wa wanawkae nchini,kuweka msisitizo wa Maadhimisho kwa mwaka husika,kutoa nafasi kwa jamii kutafakari changamoto zinazowakabili wanawake na kuzitafutia ufumbuzi,pamoja na kuelimisha Jamii kuhusu shughuli mbalimbali za wanawake 
 
Aidha risala hiyo ilizidi kusema kuwa nchi ya Tanzania ipo mstari wa mbele kwa kuwa na Mipango madhubuti ,inayoelimisha Jamii kuwa na uwiano wa Kijinsia, katika kusimamia nakugawana rasilimali zilizopatikana katika Jamii bila ya kuwa na upendeleo wa upande wowote.

 Aidha wamesema wanupongeza mkoa kwa kuendelea kuwahimiza wakurugenzi ,watendaji wa Halmashauri kutenga asilimia 10%  katika mapato yake ya ndani kwaajili ya mikopo kwa wanawake ,vijana,watu wenye ulemavu,kwa uwiano wa asilimia 2 ili kutumisha Mfuko wa Maendeleo .

Katika kuadhimisha siku hiyo wanawake mkoa wa Arusha waliweza kushiriki katika shughuli mbalimbali ikiwemo michezo,kufanya usafili katika Kituo Cha Afya Levolosi,kongamano,kutembelea mbuga za wanyama ambazo zimeleta hamasa kubwa Kwa makundi yote ya wnaawake na Jamii kwa ujumla.

Aidha Kauli mbiu hiyo inatoa nafasi  na majukumu kwa kila mtu katika nafasi yake kuapza sauti na kuchukua hatua na kutokomeza vitendo vya Ukatili ubakaji baina ya wenza ,Ukatili wa kingono Kama vile rushwa ya ngono,matusi ,ulawiti,kutupa au kutelekeza watoto ,ukeketaji ,Ukatili Dhidi ya Wanawake ukiwepo Mpango wa Taifa wa kuzuia Ukatili Dhidi ya Wanawake na watoto. 
 
Nchini Tanzania maadhimisho ya siku ya wanawake duniani,yamefanyika  kimkoa katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha yakiongozwa na Kauli Mbiu ‘Kizazi cha haki na usawa kwa maendeleo endelevu, Tujitokeze kuhesabiwa’ ambapo Mgeni Rasmi ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambayo yanafanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha akiwa katika banda la Mtandao wa Jinsia Tanzania ( TGNP). Kushoto ni Mkurugenzi wa TGNP, Bi. Lilian Liundi.
 
 Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella (katikati) kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani  ambayo yanafanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha akiwa katika banda la Mtandao wa Jinsia Tanzania ( TGNP).
Mgeni Rasmi ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella (kulia) kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambayo yanafanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha akiwa katika banda la Mtandao wa Jinsia Tanzania ( TGNP).
Mgeni Rasmi ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella (kushoto) kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambayo yanafanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha akiwa katika banda la Mtandao wa Jinsia Tanzania ( TGNP).
Mgeni Rasmi ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani kitaifa ambayo yanafanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha akielekea Jukwaa kuu kwa ajili ya kupokea maandamano ya wanawake kutoka makundi mbalimbali

 Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella  na viongozi mbalimbali wakipokea maandamano ya wanawake kutoka makundi mbalimbali kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambayo yanafanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha
Mwanamke akiendesha mtambo kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani akipita mbele ya jukwaa kuu katika viwanja wa Shekhe Amri Abeid Jijini Arusha
Wanawake wafanyakazi wa TANESCO wakipita mbele ya jukwaa kuu kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambayo yanafanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha
Askari polisi wanawake wakiingia uwanjani katika maadhimisho ya siku ya wanawake
Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa TGNP, Lilian Liundi akifuatilia matukio wakati maandamano ya wanawake yakiendelea




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...