Muonekano wa reli ya TAZARA sehemu ya Fuga-Kisaki KM 211 ambayo imesombwa na maji mkoani Morogoro.





Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa akifanya mawasiliano na wataalam mbalimbali katika kutafuta ufumbuzi wa haraka wa ukarabati wa reli ya TAZARA sehemu ya Fuga-Kisaki KM 211 ambayo imesombwa na maji hivi karibuni mkoani Morogoro.



Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa katika picha ya pamoja na Eng. Allan Singo (kulia) na Meneja wa TANROADS Mkoa wa Morogoro Eng. Alinanuswe Lazeck (kushoto), walipokagua miundombinu ya barabara na reli mkoani humo.



Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa katika picha ya pamoja na viongozi wa TAZARA alipokagua ukarabati wa reli hiyo sehemu ya Fuga-Kisaki KM 211 ambayo imesombwa na maji hivi karibuni mkoani Morogoro.

……………………….

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa ametoa siku 14 kwa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia TAZARA kukamilisha ujenzi wa daraja lililosombwa na maji katika sehemu ya Fuga-Kisaki KM 211 mkoani Morogoro.

Akizungumza mara baada ya kukagua eneo hilo Prof. Mbarawa amewataka watendaji hao kushirikiana na watendaji wenzao wa TANROADS na TRC ili eneo hilo likamilike haraka na safari za treni za mizigo na abiria ziendelee.

“Hakikisheni katika muda wa siku 7 hadi 14 sehemu hii inakamilika, ujenzi ufanyike mchana na usiku ili kuirudisha reli katika hali yake ya kawaida na hivyo kuondoa usumbufu kwa wateja wenu”, amesisistiza Prof. Mbarawa.

Reli ya TAZARA sehemu ya Fuga-Kisaki KM 211 mkoani Morogoro ilisombwa na maji Februari 14 mwaka huu na kuathiri huduma za usafiri na uchukuzi wa reli hiyo.

Mkurugenzi mkuu wa TAZARA Eng. Bruno Ching’andu amemshukuru Waziri Prof. Mbarawa kwa jitihada za kuwawezesha kupata vifaa vya kujenga daraja hilo na kumhakikishia litakamilika na huduma kurejea katika kipindi cha wiki mbili.

Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...