Na Farida Said, Michuzi Tv.
ASKARI wa jeshi la polisi wametakiwa kufanya kazi kwa waledi na kuzingatia maadili ya utumishi wa umma wawapo kazini hususani katika kipindi hiki ambacho taaifa linatekeleza miradi mikubwa ya kimkakati ikiwemo reli ya kisasa ya mwendo kasi pamoja na Bwawa la kuzalisha umeme la Mwalimu Nyerere.
Hayo wameelezwa na Mkurugenzi wa upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini, DCI, Kamishna wa Polisi Camillius Wambura, Wilayani Kilombero wakatika akifunga mafunzo ya maafisa wa Askali polisi katika chuo cha Maafisa polisi Kidatu.
Akizungumza na askari pamoja na maafisa polisi ambao wamehitimu mafunzo hayo DCI Wambura amesema ni wajibu wa kila askari polisi kuhakikisha hali ya ulinzi na usalama inahimalika wakati wote ili kuvutia wawekezaji kuja nchini kuweza kuweza katika miradi mbalimbali.
“Taifa letu lina miradi mikubwa ya kimkakati inayotarajiwa kuleta mageuzi makubwa ya kiuchumi nchini ikiwa ni pamoja na kuwavutia wawekezaji wanaotaka au kuja kuwekeza nchini, kazi yenu kubwa ni kuweka nchi katika hali ya utulivu na yenye usalama ili wawekezaji waje, kwani Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anafanya kazi kubwa sana ya kuzunguka duniani kuwashawishi wawekezaji kuja kuwekeza nchini”Alisisitiza Mkurugenzi huyo wa Upelelezi wa makosa ya Jinai nchini.
“Fanyeni kazi kwa weledi, busara itumike zaidi katika kufanya maamuzi na kuhudumia wananchi,Kumbukeni askari mmoja akiharibu, madhara yake ni makubwa mno katika nchi kwani inapelekea (Inasababisha) wananchi kukosa imani na Jeshi zima kwa kosa la mtu mmoja, hii inadhihirisha dhamana kubwa aliyopewa askari hivyo anatakiwa kuwa makini sana kuliko raia wa kawaida”Alisisitiza DCI, Wambura
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Maafisa wa Polisi Kidatu, Kamishma msaidizi wa Polisi, ACP Zarau Mpangule akabainisha mafunzo hayo ya miezi miwili yametolewa kwa askari 962 kutoka maeneo mbalimbali nchini kwa kuzingatia mafunzo ya darasani na vipindi vya nje.
Aidha amesema miongoni mwa mambo waliyojifunza ni pamoja na kazi za upolisi na utawala, uongozi, usalama barabarani, haki za binadamu na utawala bora, masuala ya unyanyasaji wa kijinsia, uzalendo na maadili ya utumishi wa umma pamoja na sharia ya makosa ya ugaidi.
Nae Mkufunzi mkuu wa Mafunzo hayo, ACP Edwin Kasekwa, akamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kutoa kibali kwa askari hao kuhudhuria mafunzo kwa kulenga watumishi waliokuwa hawajapandishwa vyeo kwa muda mrefu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...