Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula akifungua mradi wa mabwawa ya kufugia Samaki katika Chuo cha Maendeleo Ruaha, Mkoani Iringa.Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Ruaha, Godfrey Mafungu akitoa maelezo kuhusu miradi wa ufugaji wa samaki kwa Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt Zainab Chaula alipotembelea Chuo hapo kukagua miradi ya maendeleo.Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Zainab Chaula akimsikiliza Mtaalam wa Mazao ya ~Majini~ ya baharini/Mtoni/bwawani katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Ruaha, Iringa Chande Mazola kuhusu mradi wa ufugaji wa samaki unaoendeshwa na Chuo hicho.Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Zainab Chaula akiwawekea chakula Samaki katika moja ya bwawa lililopo kwenye mradi wa mabwawa ya kufugia Samaki ya Chuo cha Maendeleo Ruaha, Mkoani Iringa.Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Zainab Chaula akisalimiana na watumishi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Ruaha, Iringa alipotembelea Chuo hapo kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Zainab Chaula Dkt. Zainab Chaula akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Watumishi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Ruaha mara baada ya kufungua mradi wa mabwawa ya kufugia Samaki katika Chuo cha Maendeleo Ruaha, Mkoani Iringa.

Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WMJJWM

……………………………………………………………

Na WMJJWM Iringa

Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula amewataka watumishi wa Chuo cha Maendeleoya Jamii Ruaha kuwa wabunifu na kufanya shughuli za kuwaletea maendeleo.

Dkt. Chaula ameyasema hayo leo alipotembelea Chuoni hapo kukagua shughuli na miradi ya Maendeleo.

Dkt. Chaula amesema Vyuo vya Maendeleo ya Jamii ni chachu ya maendeleo ya nchi hivyo, vitumike kuibua vipaji vya watumishi na wahitimu ili waweze kuzalisha kwa tija na hatimaye kujiletea maendeleo kiuchumi.

Akiwa chuoni hapo, Katibu Mkuu amezindua mradi wa ufugaji wa Samaki unaolenga kutumika kwa mafunzo kwa wanachuo na wakazi wa maeneo jirani.

Akizungumza kuhusu mradi huo, Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Ruaha, Godfrey Mafungo amesema mradi unalenga kutoa elimu ya ufugaji wa Samaki kwa jamii na wanafunzi na kuwa moja ya chanzo cha mapato pale wanafunzi wanapohitimu wanapata fursa za kujiajiri na kuajiri.

Akitoa maelezo mbele ya mgeni rasmi, Mtaalam wa viumbe vya majini, Chande Mazola amesema mradi huo utaweza kuwakwamua wanajamii dhidi ya umasikini kwani wengi wao wameanzisha mabwawa ya ufugaji wa Samaki na kuweza kuuza kwenye maeneo yao na nje ya vijiji vyao ili kuongezea kipato cha mtu mmoja mmoja.

Awali akiuzungumzia uanzishwaji wa miradi, Katibu Mkuu Dkt. Chaula amesema, miradi ya aina hiyo ni mbinu mojawapo ya kumhudumia mwananchi hasa makundi maalum ambayo yanahudumiwa na Wizara kujikwamua kiuchumi.

Baadhi ya watumishi Ruaha CDTI, wamepongeza Katibu Mkuu Chaula kwa kuwapa motisha ya kazi na kuwashirikisha maono ya kupata mafanikio na kuahidi kuyafanyia kazi maelekezo na ushauri waliopewa ili kukifanya Chuo hicho kuwa Cha manufaa na cha kuleta tija kwa wanafunzi na jamii inayoizunguka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...