Na Humphrey Shao, Michuzi TV
WAKAZI wa jamii ya kabila la Wamasai waliopo eneo la Hifadhi ya Ngorongoro wameonesha wasiwasi kwa madai ya kutowaona Faru watano ambao wamekuwa na utaratibu wa kuwaona wanapokuwa kwenye malisho.
Wakizungumza na Michuzi TV na Michuzi Blog wakazi hao wamedai kwamba Faru hao wamekuwa na kawaida ya kuonekana katika maeneo ya malisho wanayopenda kwenda lakini kwa siku kadhaa hawajaona hali inayosababisha maswali mengi kuhusu walipo Faru hao.
Mmoja wa wakazi hao aliyejitambulisha kwa jina la Joseph Ole Shangai amesema kutokana na wasiwasi waliona wakazi wa Hifadhi ya Ngorongoro wakati Waziri Mkuu alipokwenda kuzungumza nao kupitia mkutano wa hadhara waliamua kumueleza Waziri Mkuu.
Kwa mujibu wa Ole Shangai ni kwamba hawakupata majibu ya moja kwa moja na jata uongozi wa Hifadhi ya Ngorongoro nao katika mkutano huo wakupata nafasi ya kutoa majibu.Hivyo wakazi hao bado wanakosa majibu ya wapi walipo Faru hao waliozoea kuwaona mara kwa mara.
Ole Shangai amewataja baadhi ya Faru ambao hawaonekani katika eneo la Kreta ni
Faru Maik 11 anayekaa maeneo ya Gorgor /kiboko pamoja na Faru Fauta 16 anayekaa Duma area ndani ya kreta na kwamba Faru huyo ana mtoto.
"Kutoonekana kwa Faru hao wakazi wa Ngorongoro tulitegemea majibu ya wapi walipo faru hao baada ya kuuliza swali mbele ya Waziri Mkuu lakini majibu hayakutolewa,"amedai.
Michuzi TV na Michuzi Blog iliamua kumtafuta Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano Hifadhi ya Ngorongoro Joyce Mgaya ili kupata ufafanuzi utakaowatoa wasiwasi wananchi ambapo amejibu kuwa Faru wote wapo ndani ya Kreta.
" Naitwa Joyce Mgaya, ni mtumishi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na kwa sasa ni Mkuu wa kitengo cha Uhusiano. Swali lako ambalo umetutumia jibu lake Faru wote wapo ndani ya Kreta."
Alipoulizwa kwanini walishindwa kutoa ufafanuzi kuhusu Faru hao walipo mbele ya Waziri Mkuu, Mgaya amejibu kwamba Protokali ya siku hiyo haikuwa imepangwa, ndiyo maana hakukuwa na majibu waliyoweza kutoa.
"Ninacho weza kusema kwa uhakika ni kwamba Faru wapo ndani ya Kreta na kwa sababu ni wanyama ambao wako kwenye maeneo yao ya asili huwa wanazunguka/ wanahama na kutembea ndani ya eneo lote, hivyo yawezekana kabisa pindi wako msituni wageni hawawaoni.Nikuhakikishie faru ndani ya kreta wapo,"amesisitiza Joyce Mgaya.
Pamoja na ufafanuzi huo mwandishi alifanya jitihada za kumtafuta Mhifadhi wa faru hao
Bajuta Sacc lakini hakupatikana.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...