*Waruhusiwa na Serikali kukopa kumalizia miradi
Na Chalila Kibuda, Michuzi Tv
Mwenyekiti wa Bodi wa Shirika la Taifa la Nyumba (NHC) Dk.Sophia Kongela Serikali inaendelea kuliimarisha Shirika kwa kulipa mtaji wa kujenga nyumba za gharama nafuu na ya kati ili watanzania wengi waweze kunufaika.
Uimarishaji huo umetokana na Serikali kutoa mkopo kwa Shirika wenye thamani ya shilingi bilioni 20 ulioliwezesha Shirika la Nyumba la Taifa kufanya ujenzi wa nyumba 1,000 katika Jiji la Dodoma ambapo hadi sasa nyumba 300 zimejengwa katika eneo la Iyumbu na nyumba 100 zinakamilika eneo la Chamwino.
Dk.Kongela ameyasema hayo leo Machi 12 , 2022 wakati wa Kikao cha Dharula cha Baraza la Wafanyakazi wa NHC lililofanyika jijini Dar es Salaam.
Kongela ameishukuru Serikali kwa kuliruhusu Shirika kukopa shilingi bilioni 173.9 ili kukamilisha miradi iliyokuwa imesimama.
Amesema kikao hicho ni muhimu cha kujadili bajeti ya Shirika kwa mwaka 2022/23 katika kufahamu kwa upande wenu mna majukumu mengi, hivyo kutenga muda wa kukutana kwa ajili ya shughuli za Baraza ni jambo linalostahili ambalo ndio nguzo ya shirika
Dk.Kongela amesema wawakilishi wa wafanyakazi kufika kwenu kunaleta uwakilishi mzuri na hasa mnapojadili masuala yenye mustakabali mkubwa kwa maendeleo ya Shirika.
Aidha amesema mipango na bajeti, inalenga kuboresha utendaji wa Sekta ya Umma kwa utoaji wa matokeo yanayotarajiwa; kuboresha kufanya maamuzi ya Shirika; kukuza uwajibikaji; kuboresha ugawaji sahihi wa rasilimali na kuhakikisha uwekaji wa vipaumbele katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku.
Amesema wakati wa mchakato wa kupanga ndipo maamuzi ya kimkakati hufanywa kuhusu changamoto za kushughulikia na namna ya kuboresha utoaji wa huduma kwa wafanyakazi na wananchi kwa ujumla hivyo, muwe na mkazo mkubwa katika kushiriki kikamilifu, kushauriana na kukubaliana juu ya mipango na malengo mliyojiwekea katika bajeti ili kuhakikisha kuwa mipango na bajeti inakuwa halisi na yenye kutekelezeka.
Hata hivyo amesema wananchi wanavyolizungumzia wanavyolizungumzia Shirika. Wengi wameongeza imani kwa huduma tunazozitoa na ndiyo maana miradi ya ukandarasi ya taasisi mbalimbali imeendelea kuongezeka kwa kiwango kikubwa.
Dk.Kongela amesema changamoto nyingi ikiwemo, kutolipwa fedha kwa wakati pindi mnapowasilisha hati za malipo, kuhitajika kulipa kodi nyingi ikiwemo kodi ya ongezeko la thamani (VAT) katika ujenzi na uuzaji wa nyumba, baadhi ya wapangaji wa Shirika kutolipa kodi kwa wakati na hivyo kulimbikiza madeni makubwa. Licha ya kukabiliana na changamoto hizo bado mmeweza kutekeleza majukumu yenu kwa ufanisi ikiwemo kuendelea kuaminiwa na Serikali kujenga majengo ya kudumu ya Wizara nane kwa awamu ya pili Jijini Dodoma
Amesema mkutano huu ni maalum kwa ajili ya kupitia utekelezaji wa bajeti ya Shirika kwa mwaka wa fedha 2021/22 na mapendekezo ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/23. Kwa kuzingatia nafasi ya Baraza la Wafanyakazi katika suala hili, ombi langu kwenu ni kwamba mtumie fursa hii kujadili kwa uhuru na uwazi suala hili. Kupitia Mkutano huu, yapatikane mapendekezo ambayo yataisaidia Shirika katika kutekeleza Mpango na Bajeti ya Shirika letu kwa ufanisi zaidi. Aidha ili kutekeleza azma ya Serikali ya Awamu ya Sita katika kuhakikisha kazi inaendelea, niwaombe majadiliano yasaidie pia kuibua mbinu na mikakati mipya ya utoaji huduma itakayosaidia kuhakikisha kazi za Serikali zinaendelea.
Ametoa wito kila mmoja wetu hasa Mameneja wa Mikoa kuhakikisha kuwa mnakusanya kodi na malimbikizo yote ili bajeti ya Shirika iliyopangwa iweze kutekelezeka na nimedokezwa kuwa moja ya sababu za kuwepo malimbikizo ni makossa yetu mbalimbali ya kiutendaji. Hatutaendelea kuvumilia utendaji wa aina hii kwa siku zijazo.
"Kodi ndio uti wa mgongo wa Shirika, hivyo tunahitaji kuwa makini na kulipa uzito suala hili. Kila mmoja wetu ahakikishe kuwa anatekeleza wajibu wake ipasavyo, ili ujenzi wa nyumba na ukusanyaji wa kodi uweze kutekelezwa kwa mafanikio makubwa. Kila mtu akitekeleze wajibu wake ipasavyo tutaweza kufika salama katika safari yetu"
Nae Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Dk.Maulidi Banyani amesema kuwa wanaendelea kujenga uwezo wafanyakazi katika kujenga ufanisi.
Aidha amesema kuwa wafanyakazi wote kufanya kazi kama timu katika kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi kwa kuwapatia makazi.
Dk.Maulidi amesema kuwa changamoto zilizotolewa na mwenyekiti wa bodi watazifanyiakazi ikiwa ni katika kuendelea kulijenga shirika
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Dk.Maulidi Banyani, akizungumza na Wafanyakazi wa shirika hilo kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti wa Bodi wakati wa kikao cha Wafanyakazi juu ya Bajeti ya Shirika hiloMwenyekiti wa Bodi wa Shirika la Taifa la Nyumba (NHC) Dk.Sophia Kongela , Akizungumza na Wafanyakazi wa NHC Juu ya Malengo waliyojiwekea kwa Mwaka 2022//2023
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Wafanyakazi wa Shirika la Nyumba wakimsikiliza Mwenyekiti wa bodi
Mwenyekiti wa Bodi wa Shirika la Taifa la Nyumba (NHC) Dk.Sophia Kongela akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Dk.Maulidi Banyani.
Mwenyekiti wa Bodi wa Shirika la Taifa la Nyumba (NHC) Dk.Sophia Kongela, akiwa katika picha ya Pamoja na Wanawake wa Shirika hilo
Mwenyekiti wa Bodi wa Shirika la Taifa la Nyumba (NHC) Dk.Sophia Kongela , akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa mkutano wa NHC
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...