Sherehe imeanza kwa kupambwa na wasanii wa kike kutoka bendi ya muziki ya wanawake ya Bahati.
Aidha, kikosi cha kutoa hamasa kutoka Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kimetoa burudani ya aina yake kwa kuwapokea wageni wote kwa burudani ya matarumbeta na ngoma.
Wadau mbalimbali wameshiriki kwenye sherehe hii ya kuchangia Twiga Stars.
Sherehe hii pia imeratibiwa na Wizara kwa kushirikiana na taasisi ya Dadahood ambayo imezindua albamu ya nyimbo ya Orange.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...