Meneja  Rasilimali Watu, Veneranda Mpaze wa Shirika la Taifa la Bima (NIC) akizungumza ma waandishi wa habari katika siku ya wanawake Duniani wakati walipoenda kutoa elimu kwa wanawake katika soko la Karume jijini Dar es Salaam.

 

*Yaahidi kwenda sambasamba na wafanyabiashara katika masoko 

Na Chalila Kibuda, Michuzi Tv

KATIKA kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani Shirika la Bima la Taifa (NIC) limewatembelea wanawake wa soko la Karume kwaajili ya kuwapatia elimu ya Bima ili kuondokana na hasara zitokanazo na majanga ya moto ambayo yakiwafika mitaji yao kufa na kuanza kuwaza mikopo waliokopa.

Kutokana na janga la moto lililowakuta wafanyabiashara wa soko la Karume NIC imefika kutoa elimu ya Bima kwa wanawake katika maadhimisho ya siku ya wanawake kwa kutaka majanga yakiwafika wanatakiwa kutabasam kwa kujua mitaji yao itarudi kutokana na kukata bima.

Akizungumza katika zoezi la utoaji elimu hiyo Meneja Rasilimali Watu, Veneranda Mpaze amesema kuwa kwa kutambua na kuthamini mchango wa Wanawake wameamua kukutana na wanawake wafanyabiashara wa soko la karume kwa kuwapa pole na kuwatia moyo waendelee na biashara zao.

Amesema NIC wanaamini katika usawa wa jinsia leo ni chachu ya maendeleo ya kesho ndiyo maana wapo kwaajili ya kuwapatia elimu ya bima na faida zake katika biashara.

“Katika Maadhimisho haya NIC natumia fursa hii kuwataarifu kwamba mnaweza kulinda biashara zenu na kuondokana na hasara za namna hii mkiwa na bima ya biashara kutoka NIC kwasababu utafidiwa kwa kurejeshewa kilichopotea endapo majanga kama haya yanatokea na wakati wote unatembea kifua mbele ”. Amesema Veneranda.

Aidha amesema unaweza ukakata bima ya biashara yako kuanzia mtaji wa shilingi 25,000 mpaka shilingi milioni 18 utalipia shilingi 59,000 na VAT ndani yake.

Ameeleza kuwa kutokana na janga hili la moto, anawasihi wanawake kuchamkia bidhaa za LINDA MJENGO ambayo inampa Mtanzania kinga dhidi ya janga la moto kwenye nyumba yake.

“Kupitia Bima hii mteja akipata janga la moto, tetemeko au mafuriko, NIC itampatia asilimia 40% ya pesa yake ndani ya siku moja ili aweze kupata makazi mbadala wakati akijiandaa kujenga nyumba nyingine kwa pesa atakayolipwa na NIC”. Ameeleza

Kwa upande wake Mwenyekiti wa soko Karume Bw.Geofrey Milonge amewapongeza NIC kuonesha moyo wa kuwajari kwa kuhakikisha wafanyabiashara wa eneo hilo wanafahamu umuhimu na faida ya kujiunga na Bima ya NIC.

Nae Mwenyekiti wa Mtaa wa Ilala Kota Bw.Amini Migomba amesema NIC wameona umuhimu wao na kuona ni jinsi gani wanaweza kuwasaidia wafanyabiashara wa soko hilo.

Amesema kupitia elimu hiyo wanayoitoa NIC kuhusu umuhimu wa Bima utasaidia wafanyabiashara wengi kujiunga na bima hiyo na kuondokana mfumo wa mwanzo wa kulialia kwa kukosa msaada.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Ilala Kota Amini Migomba akizungumza na wafanyabiashara wa Soko la Karume kuhusiana na umhimu wa Bima wakati NIC ilipofika kutoa elimu kwa wanawake katika maadhimisho ya Siku ya wanawake Duniani.
Afisa Mwandamizi wa Bima wa NIC Erica Gabriel Nnko akizungumza na wafanyabishara wa Soko la Karume wakati walipokwenda kutoa elimu kwa wafanyabishara kwa wanawake katika maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani.
Afisa Bima wa NIC  Elizabeth Chacky akizungumza na wafanyabiashara wa soko la Karume kuhusiana na umuhimu wa Bima kwa wakati wote wakati walipotembelea wafanyabiashara katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.
Baadhi ya wafanyabiashara wa soko la Karume wakipata elimu ya Bima kutoka NIC.
Baadhi ya wafanyakazi wanawake wa NIC wakiwa katika soko la Karume kwa ajili ya kutoa elimu ya bima katika maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...