Na Amiri Kilagalila,Njombe

Kitengo maalum kwa ajili ya wanafunzi wenye ulemavu katika shule ya msingi Matembwe tarafa ya Lupembe halmashauri ya wilaya ya Njombe,kinakabiliwa na changamoto lukuki hali inayopelekea kupungua kwa ufanisi wa kituo hicho.

Akizungumza na mtandao huu mwalimu wa darasasa maalum la wanafunzi wenye uhitaji Mwl.Frola Longo amesema darasa hilo lenye wanafunzi 22 wamekuwa wakikabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo wanafunzi kushindwa kuhudhuria darasani kwasababu ya umbali wanaotoka kutokana hali zao za ulemavu huku changamoto kubwa ikiwa ni uhaba wa miundombinu pamoja na ukosefu wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia.

“Kituo chetu tunakabiliwa na uhaba wa walimu,vyumba vya madarasa kwa hatua zote tatu kwani wote wapo katika darasa moja,bweni la wavulana na wasichana pamoja na mhudumu wao,Mpishi wa kuwapikia chakula kwani walimu ndio tunaowapikia,baadhi ya wanafunzi kutoka mbali na kushindwa kuhudhulia masomo”alisema Mwalimu Frola Longo

Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule ya msingi Matembwe bwana Beatus Mlela amesema bajeti ndogo inayotengwa na serikali imepeleka kushindwa kupunguza baadhi ya changamoto za kitengo hicho

“Kwa wanafunzi wa kawaida hakuna shida kubwa sana ila shida kubwa ipo kwa hawa wenzetu ambao wanamahitaji maalum,wanafunzi hawa wanamahitaji mengi sana lakini kubwa hasa ni bweni ili kuwaweka pamoja waweze kuhudumiwa vizuri maana ni changamoto kubwa kupata usafiri wanapotoka nyumbani na pili ni bajeti ndogo ya serikali katika kuhudumia hawa watoto kwasababu wanapata huduma zote hapa hapa”alisema Beatus Mlela

Kwa kuona umuhimu wa kuendelea kupunguza changamoto katika kitengo hicho,baadhi ya wadau kutoka mashirika yasiyo ya kiserikali ikiwemo shirika la COCODA,shirika la SAFINA pamoja na wataalumu kutoka halmashauri ya wilaya ya Njombe wametembelea shule hiyo na kutoa baadhi ya vifaa vya kufundishia wanafunzi hao.

“Sisi tunafanya kazi na jamii kwa kutoa misaada mbali mbali ikiwemo kusaidia watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu kwa hiyo tunashukuru sana kwa kujumuika hapa kwa kuwatembelea watoto na kutoa chochote ili tuweze kupunguza changamoto kwa kuwa leo tumekuja kujifunza”alisea Violeth Milinga muwakilishi wa shirika la COCODA

“Kwanza ninashukuru kwa kufika hapa kuliko ningeskia tu kuna shule ya wanafunzi maalum,tumeiona hali ya wenzetu na mahitaji wanayoyahitaji.Tunawashukuru wazazi waliowaonyesha watoto hawa ili waweze kupata elimu lakini pia serikali yetu kwa kutenga kitengo hiki nan i vema ikafanyika hata kwa shule zingine”aliseama Gracanna Ndonde katibu wa shirika la SAFINA kwa niaba ya Mkurugenzi.

Iren Ndende ni afisa elimu maalum wa halmashauri ya wilaya ya Njombe amesema serikali imekuwa ikitekeleza baadhi ya majukumu kwa awamu ikiwemo kusambaza vifaa vya kujifunzia na kufundishia kutokana na umuhimu wa kitengo hicho katika maeneo mbali mbali.

“Serikali inatambua uwepo wa watoto wenye mahitaji maalum na kuona umuhimu wa kutatua changamoto zao ikiwa ni pamoja na kusambaza vifaa vya kujifunzia na kufundishia lakini pia vifaa saidizi.Serikali inafanya hilo kwa awamu kwa hiyo tunaamini katika halmashauri yetu tutapata pia vifaa”alisema Iren Ndende

Kwa upande wake Debora Nsemwa afisa maendeleo ya jamii halmashauri ya wilaya ya Njombe kwa niaba ya mkurugenzi wa halmashauri hiyo,ameipongea idara ya elimu kuendelea kushughulika na kitengo hicho na kuahidi kufikisha kwa mkurugenzi ili kuendelea kupunguza changamoto hizo.

“Kwa kweli tunawpongeza waalimu wa kitengo hiki kwa kazi kubwa wanayoifanya lakini pia tumefurahi kuona mafanikio yaliyotajwa ikiwemo wazazi kuwa na mtizamo chanya juu ya watoto wa namna hii,na ninaamini changamoto zilizopo nimeziskia nitafikisha katika ngazi nyingine”alisema Debora Nsemwa

Kitengo hicho maalum katika shule ya msingi Matembwe kilianzishwa mwaka 2016 kikiwa na wanafunzi watatu na sasa kimefikisha idadi ya wanafunzi 22 huko lengo kubwa la kitengo hicho pia ikiwa ni kufundisha stadi za maisha kwa watoto wenye ulemavu.

Baadhi ya wanafunzi pamoja wenye mahitaji maalum wakiwa kwenye picha ya pamoja na wawakilishi kutoka mashirika binafsi pamoja na wataalum wa serikali baada ya kukabidhi vifaa mbalimbali kwa ajili ya kujifunza na kufundishia.
Baadhi ya wanafunzi wakiwa katika darasa lao wakati walipotembelewa na baadhi ya wadau kwa ajili ya kupewa msaada.

Baadhi ya vifaa vya msaada vilivyokabidhiwa na wadau kwa kushirikiana na serikali ili kusaidia kitengo cha wanafunzi wenye mahitaji maalum.



 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...