Na. WAF - Dar es Salaam

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amewataka watanzania wanaotumia usafiri wa bodaboda kuwa makini ili kupunguza ajali zinazopelekea kupoteza viungo vya mwili.

Ameyasema hayo leo Machi 21, 2022 Wakati akifungua mafunzo ya wataalamu wa upasuaji wa ubongo, uti wa mgongo pamoja na wagonjwa mahututi yanayofanyika katika taasisi ya mifupa ya MOI jijini Dar es Salaam.

Waziri Ummy amesema mafunzo hayo yamekuja kwa wakati, kwa sababu Tanzania inashuhudia ongezeko la upasuaji wa mifupa, uti wa mgongo pamoja na magonjwa ya mishipa ya fahamu kutokana na ajali mbalimbali ikiwa ni pamoja na bodaboda.

"Sio jambo jema kwa Bodaboda kuanza kujifunza kuendesha pikipiki leo na kesho anaingia barabarani kuchukua abiria, ajali nyingi zinasababishwa na uzembe na kutofuata sheria za barabarani". Amesema Waziri Ummy.

"Tutakaa na wenzetu wa Wizara ya mambo ya ndani kuhakikisha tunatafuta ufumbuzi wa hili ili kupunguza ajali za uzembe zinazoweza kuepukika kwa kuwa watu wengi wamekuwa wakipoteza viungo vyao vya mwili kwa kuvunjika na kuwekewa vya bandia." Amesema Waziri Ummy.

Mafunzo hayo yanaendeshwa na watanzania kwa kushirikiana na wataalamu kutoka nchini Marekani, Australia pamoja na Canada na lengo la mafunzo hayo ni kuongeza ujuzi, uzoefu na utaalamu.

Katika hatua nyingine Waziri Ummy ameendelea kuwasihi watanzania kujitokeza kupata chanjo ya UVIKO-19 kwa kuwa bado Corona ipo Tanzania.

Pia amesema shirika la Afya Duniani limethibitisha kuwa kuna kirusi kipya cha Corona kimegundulika ambacho Delta kimechanganyana na Omicron na kinatambulika kwa jina la Omicron.DA1

"Serikali imeshachukua hatua za kuendelea kuchunguza na kujua kwamba kimeingia Tanzania au bado lakini nchi nyingine tayari wameshathibitisha." Amesema Waziri Ummy.

Hivyo amewata watanzania kuendelea kuchukua tahadhari kama wanavyoelekeza wataalamu ikiwepo kunawa mikono kwa maji tiririka na kuvaa barakoa. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...