Balozi wa Marekani nchini Mhe. Dkt. Donald Wright amepongeza uendeshaji wa michakato ya kisiasa inavyoendeshwa nchini Tanzania.

Balozi Wright ameyasema hayo wakati alipokutana kwa mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Balozi Wright amesema anaridhishwa na jinsi hali ya kisiasa ilivyo hapa nchini na kuongeza kuwa anaunga mkono michakato ya kisiasa inavyoendeshwa nchini na kuelezea kuridhishwa kwake na hali hiyo.

Pamoja na mambo mengine, viongozi hao wamejadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Marekani kwa maslahi ya pande zote mbili.

Naye Waziri Mulamula amemuahidi Dkt. Wright kuwa Serikali itaendelea kutoa ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yake wakati wote hapa nchini.

Katika tukio jingine, Waziri Mulamula amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Norway nchini Mhe. Elisabeth Jacobsen na kujadili masuala ya ushirikiano katika masuala ya amani na usalama, jinsia na uwezeshaji wa wanawake.

Pia, Waziri Mulamula amekutana kwa mazungumzo na Afisa kutoka Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) Bibi. Jacqueline Machangu-Motcho na kujadili masuala ya ushirikiano baina ya mfuko huo na Tanzania.


Balozi wa Marekani nchini Mhe. Dkt. Donald Wright akiongea na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akimueleza jambo Balozi wa Marekani nchini Mhe. Dkt. Donald Wright


Kikao cha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula na Balozi wa Marekani nchini Mhe. Dkt. Donald Wright kikiendelea


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Balozi wa Norway nchini Mhe. Elisabeth Jacobsen katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akizungumza Afisa kutoka Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) Bibi. Jacqueline Machangu-Motcho katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...