Na.Mwandishi wetu, Michuzi Tv

KLABU ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi Watanzania 'JWTZ' ya Lugalo Gofu imefungua rasmi mwaka wa Mashindano ya Mchezo Wa Gofu Kwa Mwaka 2022, katika sherehe Ya Kufunga Shinda La Combat Fiddle lililofanyika kwenye Viwanja vya klabu hiyo.

Akizungumza kwenye Hafla fupi ya ufungaji wa Shindano hilo maalum lililoandaliwa kwa lengo la kuwapongeza Maafisa wa Jeshi waliopanda Cheo Mwenyekiti wa klabu Brig.jenerali mstaafu Michael Luwongo,Amewapongeza Maafisa hao kwa hatua waliopiga na kuwa msaada kwa Jeshi na Taifa kiujumla.

 Kwa upande wake Nahodha wa klabu hiyo  Meja Japhet Masai Ametoa neno la Shukrani kwa niaba ya maafisa wote na kuahidi ushirikiano katika kukuza Mchezo wa Gofu Tanzania.

Akieleza kukamilika kwa asilimia 90 maandalizi ya Shindano La "European Tour" Katibu wa chama cha Mchezo wa Gofu Tanzania Eng.Enock Magile,Amesema Wanatarajia ujio wa wachezaji kutoka mataifa mbalimbali.

Aidha,Wachezaji Mbalimbali wameibuka kinara kwenye shinda hilo huku Mchezaji Peter Fiwa Akiwa kinara kwa ushindi wa Jumla kwa pointi 36,washindi wengine wa divisheni A Eng.Enock Magile na Samuel Kileo,Divisheni B saki Opuku na Erick Tango wakifanya vizuri Kwa Divisheni C  Nsagwa Mwasasu na Nassan Mpangala kwa upande wa wanawake Evelyne Atukunda na Evelyne Ngweshemi Wakifanya vizuri zaidi.

Mwenyekiti wa klabu ya Lugalo Gofu,Brig.Jenerali Michael Luwongo Wakati Akizungumza kwenye hafla ya kufunga shindano la Combat Fiddle Lililofanyika Kwenye Viwanja vya klabu hiyo kwa ajili ya kuwapongeza maafisa wa Jeshi waliopanda Vyeo.
Mwenyekiti wa klabu Brig.Jenerali Mstaafu Michael Luwongo (Upande wa kulia) akimkabidhi Mshindi wa Jumla,Peter Fiwa upande wa  kushoto akipokea zawadi yake mara baada ya kutangazwa mshindi kwenye shindano la Combat Fiddle Lililofanyika Kwenye Viwanja vya klabu ya Lugalo Gofu.
Mchezaji Samuel Kileo kutoka klabu ya Lugalo Gofu akipokea zawadi yake ya mshindi wa pili wa Divisheni A,mara Baada ya Kutangazwa mshindi kwenye shindano la Combat Fiddle Lililofanyika Kwenye Viwanja vya klabu hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...