Benki ya Exim Tanzania hii leo imeungana na Dunia kwa ujumla katika kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani. Katika kuadhimisha siku hiyo muhimu viongozi waandamizi wa benki hiyo wakiongozwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo Bw Jaffari Matundu walipata fursa ya kufurahi pamoja na kujadili mambo mbalimbali na wafanyakazi wa benki hiyo ikiwemo kuhamasisha usawa wa kijinsia katika uendeshaji wa benki hiyo.

Katika mazungumzo yake na wafanyakazi hao Bw Matundu alisema benki hiyo inachukulia kwa umuhimu mkubwa suala la usawa wa kijinsia sambamba na kuwawezesha wanawake katika nyanja mbalimbali ikiwemo suala zima la ajira.

“Kipaumbele kwa wanawake katika benki ya Exim hakiishii tu kwa wafanyakazi wetu bali pia wateja wetu. Tumekuwa tukifanya jitihada za makusudi katika kuinua ustawi wa wanawake kupitia huduma zetu tunazozitoa ikiwemo mikopo na mafunzo ya kibiashara,’’ alisema.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim Bw Jaffari Matundu (Katikati) pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo wakionesha ishara ya kuvunja upendeleo wa kijinsia (Break the bias) ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani. Benki hiyo imeungana na Dunia katika kuadhimisha siku hiyo muhimu kupitia hafla fupi iliyofanyika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam leo.


Wafanyakazi mbalimbali wa Benki ya Exim Tanzania wakionesha ishara ya kuvunja upendeleo wa kijinsia (Break the bias) ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...