Mkurugenzi wa Kampuni ya Blanq Amin Swai akizungumza na waalikwa katika semina ya iliyojumuisha wawakilishi wa vyombo vya Habari iliyofanyika jijini Dar essalaam.

Na.Khadija Seif, Michuzi TV

WAMILIKI wa vyombo vya Habari wameshauriwa kuboresha Mifumo na kuongeza ubunifu Ili waweze kufanya kazi na Makampuni mbalimbali.

Akizungumza na Michuzi TV wakati wa kufungua Semina ambayo imewajumuisha Taasisi mbalimbali Pamoja na waamiliki wa vyombo vya Habari, Mkurugenzi wa Kampuni ya Blanq Amin Swai amesema ni wakati wa wamiliki wa vyombo vya Habari kuongeza ubunifu Ili kuendana na Kasi iliyopo na Kufahamu jamii inahitaji Mfumo upi.

Hata hivyo Swai, ameeleza Kwa jinsi gani Masoko mapya yanavokuja Kwa Kasi hususani Soko la Wanawake pamoja na wapambanaji na Wafanyabiashara wadogo wadogo.

Aidha ametoa wito Kwa Waandishi Wahabari Kwa namna gani waweze kuhabarisha jamii katika habari za Majanga na Matukio ya kutisha ili waweze kutoa ushauri kwa jinsi gani msaada unaweza tolewa kwa wakati huo kwenye janga hilo.
Baadhi ya wawakilishi na wadau wa vyombo vya Habari wakisikiliza Kwa makini taarifa inayowasilishwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Blanq nchini Amin Swai wakati wa semina. iliyoandaliwa na internews jijini Dar es salaam.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...