Na Khadija Kalili , Kibaha

Kamati ya Amani ya Mkoa wa Pwani inatarajia kufanya kongamano kubwa la ibada ya kuiombea serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais
Samia Suluhu Hassan litakalohusisha waumini wa dini mbalimbali zaidi ya 200 litafanyika kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani maandalizi yamekamilika.

Akizungumza katika mkutano na Waandishi wa Habari Mkoani hapa Mwenyekiti Mwenza wa Kamati hiyo ambaye pia ni Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Pwani Hamisi Mtuoa alisema kuwa viongozi wa dini kwa kupitia Kamati hiyo wamekubaliana kuwa mwezi Machi uwe mwezi wa maombi kwa kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan ambaye anatimiza mwaka.mmoja tangu aingie madarakani katika awamu ya sita.

"Tutaiombea nchi yetu iepushwe na majanga mbalimbali ya uvunjifu wa amani pia sisi kama viongozi wa dini tunao wajibu wawa kumuombea Rais wetu ,nchi yetu na dunziama kwa ujumla kongamano hilo limepangwa kufanyika Machi 14 na litawakutanisha watu maarufu, viongozi kutoka katika Wilaya zote za Mkoa wa Pwani"alisema Sheikh Mtupa.

Alisema kuwa "Viongozi wa dini tunao wajibu wa kuomba dua kupongeza mambo yotemazuri aliyoyafanya Rais wetu Mama Samia, viongozi wa dini tunatakiwa kuzisemea changamoto zilizopo pia kuinua mikono kumuombea Rais wetu huu ni muda sahihi kwetu tumuombe Mungu atuondoshee majanga mbalimbali yanatokea katika nchi za wenzetu Ukraine na Urusi na kuifanya Tanzania iwe kisiwa cha amani duniani".

Pia katika kongamano hilo tuta endelea kutoa hamasa za chanjo waumini wetu wanapaswa kuitikia wito wa kuchanja Ili kujikinga na na ugonjwa Uviko 19.

Pia tutahamasisha wakaazi wa Mkoa wa Pwani kuhamasisha waamini wetu kushiriki katika sensa ya makazi itakayofanyika mwezi Agosti mwaka huu hili zoezi ni muhimu sana .

Akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti Mwenza Kamati ya Amani Mkoa wa Pwani Padri Benno Kikudo wa Kanisa Katoliki Parokia ya Tumbi Kibaha Mchungaji Emmanuel Muhina alisema kuwa anawaalika watu mashuhuri ndani ya Mkoa wa Pwani kuungana na Kamati hiyo Ili waweze kufanya maombi ya kuiombea amani nchi nzima kwa ujumla.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakar Kunenge ndiye atakaye kuwa mgeni rasmi siku hiyo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...