Na Mwandishi Wetu

Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetembelea kiwanda cha bia cha Kampuni ya Serengeti (SBL) cha Dar es Salaam  na kuelezea kuridhishwa na uwekezaji inayofanya kampuni hiyo hapa nchini.

Akiongea katika ziara hiyo iliyolenga kuangalia namna zoezi la utekelezaji wa stempu za kielekroniki unavyoendelea, mwenyekiti wa bodi hiyo Ulledi Mussa alisema uwekezaji unafanywa na SBL unatija kubwa kwa taifa.

“Upanuzi mkubwa wa viwanda vyenu unaonyesha kuwa mpo na mtanendelea kuwepo. Serikali ipo Nyuma yenu na changamoto mbali mbali za kikodi zzitakuwa zikendelea kufanyiwa kazi ili kuwawekea mazingira mazuri zaidi ya kufanya kazi,” alisema

Mwenyekiti huyo alisema kuwa TRA inaichukulia kampuni ya SBL km mdau muhimu wa maendeleo na kushukuru kwa uwekezaji wake katika miradi mbali mbali ya kijamii.

Kwa upande wake, mkurugenzi wa mahusiano kwa umma wa SBL John Wanyancha alisema kampuni hiyo imekuwa ikiwekeza katika midari mbali mbali ya kijamii kama vile maji, elimu, Kilimo endelevu na nyinginezo.

Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Bia ya SBL Mark Ocitti (kushoto) akiongea na wajumbe wa bodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)  muda mfupi kabla ya ziara ya kutembelea kiwanda cha SBL Dar es Salaam kuangalia namnamfumo wa stempu za kielekroniki unavyofanya kazi.

Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Bia ya SBL Mark Ocitti (kushoto) akiongea na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Alphayo Kidata muda mfupi kabla ya ziara ya kutembelea kiwanda cha SBL Dar iliyofanywa na wajumbe wa bodi ya TRA.

Meneja wa kiwanda cha bia cha SBL Dar es Salaam Shekar Masakare akiwaonyesha wajumbe wa bodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)  namna mfumo wa stempu za kielekroniki unavyofanya kazi wakati wa ziara yao ya kutembelea kiwanda.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...