Brigedia Jenerali Hashim Yusuf Komba ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Tanzania Automotive Technology Center (TATC),Kamanda wa Kikosi Cha Nyumbu Project kilichopo Wilayani Kibaha Mkoani


Meja Simon Rwegoshora ambaye ni Mkurugenzi Uzalishaji Shirika la Nyumbu akionesha mashine mbalimbali zilizozalishwa na kiwanda cha Nyumbu kilichopo Kibaha Mkoani Pwani wakati wa ziara ya waandishi wa habari katika ziara kiwandani hapo.
Na Khadija Kalili,Kibaha
BRIGEDIA Jenerali Hashim Yusuf Komba ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Tanzania Automotive Technology Center (TATC),Kamanda wa Kikosi Cha Nyumbu Project kilichopo Wilayani Kibaha Mkoani ametoa Rai kwa watanzania na viongozi wa dini kuzidisha maombi kufuatia vita vinavyoendele kati ya nchi ya Ukraine na Urusi.

Brigedia Jenerali Komba alitoa rai hiyo alipokuwa Akizungumza na wanahabari ambao walialikwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)ambapo waliandaliwa ziara hiyo Maalumu ya kutembelea ili shughuli mbalimbali zinazofanyika katika Kikosi hicho Cha Nyumbu ukiwa ni katika kutimiza mwaka mmoja wa kuwa madarakani Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.

Brigedia Jenerali Komba aliianisha kwa kusema kuwa ndani ya Kikosi hicho wana miradi mikubwa Saba huku baadhi ikiwa ni pamoja na uundaji wa magari, mafundi mchundo, uyeyushaji wa vyuma, pia wanakarabati magari ya kijeshi aina ya deraya ambayo huwa Yana mlinda mwanajeshi asiweze kudhurika pindi anapokuwa vitani.

Aidha Brigedia Jenerali Komba alisema kuwa Shirika Hilo la Nyumbu liliasisiwa na Rais wa Kwanza wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarege Nyerere mwaka 1977 huku alisema kuwa eneo lao linaukubwa wa Hekta 732.

Akifafanua kuhusu changamoto za uvamizi wa eneo lao Brigedia Jenerali alisema kuwa changamoto za uvamizi hazikwepeki hivyo wao huzitatua kwa Njia ya mazungumzo, huwa wanazungumza na Halmashauri ya Kibaha na Viongozi wa maeneo jirani na hivi Sasa tayari Halmashauri imeshafika kulipia eneo lao na ramani ya Shirika imechorwa.

Brigedia Jenerali Komba alisema kuwa changamoto zingine wanazozipitia kwa Sasa ni uchakavu wa majengo na upungufu wa mioundombinu pamoja na rasilimali watu.

"Tunahitaji fungu kubwa la fedha za maendeleo kuajiri Wafanyakazi kwani mapengo yapo ili kujaza nafasi za watu kwani tunahitaji Wafanyakazi waajiriwe Ili kuziba nafasi katik maeneo mbalimbali muhimu." Alisema Brigedia Jenerali Komba.

Brigedia Jenerali Komba alisisitiza kwa kusema kuwa Shirika la Nyumbu hivi Sasa limeanza kujiimarisha kwa kuendeleza miradi mama licha ya kuwa kuna changamoto wanazozipitia.

Meja Simon Rwegoshora ambaye ni Mkurugenzi Uzalishaji Shirika la Nyumbu alisema kuwa tayari wamesha pokea oda na kukarabati magai ya Kikosi Cha Zimamoto,pia wameshaunda magari hayo ambapo gari moja lina uwezo wa kukimba mwendo kasi wa farasi 250 likiwa lineundwa katika mfumo wa Kijerumani ambapo gari moja linauzwa kwa Mil.900 kwa beii ya ndani lakini endapo litanu ukiwa kutoka nje ya nchi litanunuliwa kwa Bil.1.4.

"Nashauri tupende vya kwetu na wananchi wanakaribishwa kuja kupata huduma ndani ya karakana zetu kwa sababu tunatengeneza na kukarabati magari kwa bei zenye unafuu"alisema Meja Rwegoshora.

"Tayari Shirika la Nyumbu tumetengeneza gari aina ya Four-wheeler drive la Askari, mizigo na uwanja wa vita, pia tumetengeneza gari aina ya Mark Twelve , vyoo vya kisasa vinavyotembea (Mobile Toilets) vinaweza kutumika vitani na hata katika mikusanyiko mbalimbali ya kijamii kama vile kwa wahubiri, mikutano mbalimbali"alisema Rwegoshora.

Katika ziara hiyo pia wanahabari walioneshwa Shirika lilivyo jipanga kuitengeneza nguzo za umeme za chuma ambazo zitawekewa madini ya Zink ikiwa ni katika kuzuia zisiharibike na kutu,pia Kuna mashine za kufyatua matofali ya bei nafuu ambayo Mwananchi wa kawaida anaweza kumudu, ujenzi wa majiko yenye kutumia mafuta na mkaa mashine za kupukuchua mahindi na kuchakata katani ambazo wataziuza kwa wakulima.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...