Meneja Mradi wa Usafi wa Mazingira Mjini wa Shirika la SNV,Bw. Olivier Germain akielezea kuhusu ujenzi wa Choo cha Kisasa cha umma pamoja na Mtambo wa Gesi asilia (Bio – Gas Plant) katika Kituo cha Mabasi Mkoa wa Shinyanga.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko amefungua Choo cha Kisasa cha umma pamoja na Mtambo wa Gesi asilia (Bio – Gas Plant) katika Kituo cha Mabasi Mkoa wa Shinyanga vilivyojengwa na Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV – Netherlands Development Organization) na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kupitia Mradi wa Usafi wa Mazingira (WASH SDG) na kufadhiliwa na Serikali ya Uholanzi.
Uzinduzi wa Choo cha Kisasa cha umma pamoja na Mtambo wa Gesi asilia (Bio – Gas Plant) katika Kituo cha Mabasi Mkoa wa Shinyanga (Ibinzamata) umefanyika leo Jumatano Machi 23,2022 na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa afya na mazingira wakiongozwa na Katibu Tawala Wilaya ya Shinyanga Mhe. Boniphace Chambi kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko.
Meneja Mradi wa Usafi wa Mazingira Mjini wa Shirika la Maendeleo la Uholanzi, Bw. Olivier Germain amesema ujenzi wa Choo cha Kisasa cha umma pamoja na Mtambo wa Gesi asilia (Bio – Gas Plant) katika Kituo cha Mabasi Mkoa wa Shinyanga ulioanza Mwezi Oktoba 2021 na kumalizika Mwezi Machi 2022 umetumia zaidi ya shilingi Milioni 160.
Ameyataja maeneo muhimu ya mradi huo kuwa ni vyumba vya choo kwa ajili ya wanaume na wanawake ambavyo pia vina sehemu kwa ajili ya watu wenye mahitaji maalumu (Kama vile walemavu, wajawazito, wagonjwa, watoto, wazee nk) Mabafu ya kuogea na vyumba vya kubadilishia nguo, sehemu za haja ndogo kwa wanaume (Urinals), Mashine maalumu ya kuuzia taulo za kike (Pads-Vending Mashine) zitakazouzwa kwa shilingi 200/= katika eneo la vyumba vya wanawake.
Germain amezitaja sehemu zingine kuwa ni Mtambo wa Gesi asilia (Bio – Gas Plant), Maduka na mgahawa pamoja na mfumo wa kuvuna maji ya mvua.
Germain amewasihi watumiaji wa choo hicho cha kisasa kuzingatia suala la usafi, ulinzi wa kila mmoja wa miundombinu ya choo, pamoja na kutumia choo hicho kwa ajili ya kupata gesi asilia.
“Naomba mtumie na kutunza mradi huu ili uwe endelevu, tumieni ili tupate pia gesi asilia. Choo hiki ni kwa ajili ya kila mtu kwani tumejenga kulingana na mahitaji ya watu wote wakiwemo wenye ulemavu, watoto na wazee lakini kuna chumba cha kujistiri kwa akina mama na taulo za kike ‘pedi’ zinapatikana ndani ya choo hiki bora na nafikiri hakuna choo cha namna hii hapa Tanzania”,amesema Germain.
Akizindua mradi huo kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko, Katibu Tawala wilaya ya Shinyanga Mhe. Boniphace Chambi amelishukuru Shirika la SNV kwa kushirikiana na Manispaa ya Shinyanga na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) kwa kujenga choo hicho cha kisasa na Mtambo wa Gesi asilia na kwamba mradi huo utakuwa shamba darasa na utatumika kuiingizia mapato halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
“Naomba tuutunze mradi huu ili uwe endelevu. Mradi huu ni shamba darasa na tutautumia kujifunza mambo mengi ikiwemo masuala ya usafi na matumizi ya gesi asilia. Lakini pia ndani ya Jengo hili kuna vyumba vya biashara na mgahawa ambavyo vyote vitachangia katika kuiingizia mapato Manispaa ya Shinyanga”,amesema Chambi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Jomaary Satura ameahidi kutunza mradi huo na kuwataka wadau wanaofanya shughuli zao katika Kituo cha mabasi kushirikiana kutunza mradi huo.
“Tuwashukuru wenzetu SNV kwa mradi huu na mradi mingine wanayotekeleza katika Manispaa yetu. Sisi dhamira yetu ni kuona Manispaa ya Shinyanga inakuwa kinara wa utunzaji mazingira nchini. Choo hiki kitakuwa kielelezo cha ustaarabu wetu na tayari tumefunga taa katika Stendi hii hivyo wananchi wataweza kufanya shughuli zao usiku na mchana”,amesema Satura.
Naye Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko na Diwani wa Viti Maalumu Mhe. Shella Mshandete wameipongeza SNV kujenga choo bora na cha kisasa kinachozingatia mahitaji ya watu wote wakiwemo wenye ulemavu, watoto na wanawake.
Muonekano wa sehemu ya mbele ya Choo cha Kisasa cha umma pamoja na Mtambo wa Gesi asilia (Bio – Gas Plant) katika Kituo cha Mabasi Mkoa wa Shinyanga vilivyojengwa na Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV) na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kupitia Mradi wa Usafi wa Mazingira (WASH SDG) na kufadhiliwa na Serikali ya Uholanzi. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Katibu Tawala Wilaya ya Shinyanga Mhe. Boniphace Chambi kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (katikati) akizindua Choo cha Kisasa cha umma pamoja na Mtambo wa Gesi asilia (Bio – Gas Plant) katika Kituo cha Mabasi Mkoa wa Shinyanga vilivyojengwa na Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV) na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga. Wa pili kushoto ni Meneja Mradi wa Usafi wa Mazingira Mjini wa Shirika la SNV,Bw. Olivier Germain.
Katibu Tawala Wilaya ya Shinyanga Mhe. Boniphace Chambi (katikati kulia) akisoma maandishi baada ya kuzindua Choo cha Kisasa cha umma pamoja na Mtambo wa Gesi asilia (Bio – Gas Plant) katika Kituo cha Mabasi Mkoa wa Shinyanga vilivyojengwa na Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV) na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga. Anayepiga makofi kushoto ni Meneja Mradi wa Usafi wa Mazingira Mjini wa Shirika la SNV,Bw. Olivier Germain.
Maandishi katika Choo cha Kisasa cha umma pamoja na Mtambo wa Gesi asilia (Bio – Gas Plant) katika Kituo cha Mabasi Mkoa wa Shinyanga vilivyojengwa na Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV) na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kupitia Mradi wa Usafi wa Mazingira (WASH SDG) na kufadhiliwa na Serikali ya Uholanzi.
Wananchi wakifuatilia uzinduzi wa Choo cha Kisasa cha umma pamoja na Mtambo wa Gesi asilia (Bio – Gas Plant) katika Kituo cha Mabasi Mkoa wa Shinyanga vilivyojengwa na Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV) na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kupitia Mradi wa Usafi wa Mazingira (WASH SDG) na kufadhiliwa na Serikali ya Uholanzi.
Katibu Tawala Wilaya ya Shinyanga Mhe. Boniphace Chambi kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (katikati) akikata utepe wakati akizindua Choo cha Kisasa cha umma pamoja na Mtambo wa Gesi asilia (Bio – Gas Plant) katika Kituo cha Mabasi Mkoa wa Shinyanga vilivyojengwa na Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV) na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Meneja Mradi wa Usafi wa Mazingira Mjini wa Shirika la SNV,Bw. Olivier Germain akielezea kuhusu ujenzi wa Choo cha Kisasa cha umma pamoja na Mtambo wa Gesi asilia (Bio – Gas Plant) katika Kituo cha Mabasi Mkoa wa Shinyanga.
Mhandisi wa Shirika la SNV, Hezron Magambo akielezea kuhusu ujenzi wa Choo cha Kisasa cha umma pamoja na Mtambo wa Gesi asilia (Bio – Gas Plant) katika Kituo cha Mabasi Mkoa wa Shinyanga.
Muonekano wa sehemu ya Choo cha Kisasa cha umma pamoja na Mtambo wa Gesi asilia (Bio – Gas Plant) katika Kituo cha Mabasi Mkoa wa Shinyanga vilivyojengwa na Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV) na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kupitia Mradi wa Usafi wa Mazingira (WASH SDG).
Muonekano wa sehemu ya Choo cha Kisasa cha umma pamoja na Mtambo wa Gesi asilia (Bio – Gas Plant) katika Kituo cha Mabasi Mkoa wa Shinyanga vilivyojengwa na Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV) na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kupitia Mradi wa Usafi wa Mazingira (WASH SDG).
Muonekano wa sehemu ya Choo cha Kisasa cha umma pamoja na Mtambo wa Gesi asilia (Bio – Gas Plant) katika Kituo cha Mabasi Mkoa wa Shinyanga vilivyojengwa na Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV) na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kupitia Mradi wa Usafi wa Mazingira (WASH SDG).
Muonekano wa sehemu ya Choo cha Kisasa cha umma pamoja na Mtambo wa Gesi asilia (Bio – Gas Plant) katika Kituo cha Mabasi Mkoa wa Shinyanga vilivyojengwa na Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV) na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kupitia Mradi wa Usafi wa Mazingira (WASH SDG).
Muonekano wa sehemu ya maduka katika Choo cha Kisasa cha umma pamoja na Mtambo wa Gesi asilia (Bio – Gas Plant) katika Kituo cha Mabasi Mkoa wa Shinyanga vilivyojengwa na Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV) na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kupitia Mradi wa Usafi wa Mazingira (WASH SDG).
Afisa Afya Manispaa ya Shinyanga Sanya Anthony (aliyeshikilia kipaza sauti katikati) akielezea kuhusu ujenzi wa Choo cha Kisasa cha umma pamoja na Mtambo wa Gesi asilia (Bio – Gas Plant) katika Kituo cha Mabasi Mkoa wa Shinyanga vilivyojengwa na Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV) na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kupitia Mradi wa Usafi wa Mazingira (WASH SDG).
Afisa Afya Manispaa ya Shinyanga Sanya Anthony (kulia) akielezea mfumo wa Gesi asilia katika Choo cha Kisasa cha umma pamoja na Mtambo wa Gesi asilia (Bio – Gas Plant) katika Kituo cha Mabasi Mkoa wa Shinyanga vilivyojengwa na Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV) na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kupitia Mradi wa Usafi wa Mazingira (WASH SDG).
Katibu Tawala Wilaya ya Shinyanga Mhe. Boniphace Chambi (kushoto) akinawa mikono baada ya kuingia ndani ya Choo cha Kisasa cha umma katika Kituo cha Mabasi Mkoa wa Shinyanga kilichojengwa na Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV) na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kupitia Mradi wa Usafi wa Mazingira (WASH SDG). Kulia ni Meneja Mradi wa Usafi wa Mazingira Mjini wa Shirika la SNV,Bw. Olivier Germain.
Katibu Tawala Wilaya ya Shinyanga Mhe. Boniphace Chambi akiangalia choo kwa ajili ya watu wenye mahitaji maalumu ndani ya Choo cha Kisasa cha umma katika Kituo cha Mabasi Mkoa wa Shinyanga kilichojengwa na Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV) na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kupitia Mradi wa Usafi wa Mazingira (WASH SDG). Kulia ni Meneja Mradi wa Usafi wa Mazingira Mjini wa Shirika la SNV,Bw. Olivier Germain.
Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Shinyanga Angel Mwaipopo akimwelezea Katibu Tawala Wilaya ya Shinyanga Mhe. Boniphace Chambi kuhusu Mashine ya kununulia Taulo za kike kwa shilingi 200/= tu katika eneo la vyumba kwa ajili ya wanawake ndani ya Choo cha Kisasa cha umma katika Kituo cha Mabasi Mkoa wa Shinyanga kilichojengwa na Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV) na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kupitia Mradi wa Usafi wa Mazingira (WASH SDG).
Wadau wakiwa katika eneo la kununulia Taulo za kike kwa shilingi 200/= tu katika eneo la vyumba kwa ajili ya wanawake ndani ya Choo cha Kisasa cha umma katika Kituo cha Mabasi Mkoa wa Shinyanga.
Katibu Tawala Wilaya ya Shinyanga Mhe. Boniphace Chambi (wa tatu kushoto) akizungumza jambo katika sehemu ya haja kwa wanaume ndani ya Choo cha Kisasa cha umma katika Kituo cha Mabasi Mkoa wa Shinyanga kilichojengwa na Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV) na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kupitia Mradi wa Usafi wa Mazingira (WASH SDG).
Moja ya vyumba katika Choo cha Kisasa cha umma katika Kituo cha Mabasi Mkoa wa Shinyanga kilichojengwa na Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV) na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kupitia Mradi wa Usafi wa Mazingira (WASH SDG).
Sehemu ya kunawia mikono eneo la wanaume katika Choo cha Kisasa cha umma katika Kituo cha Mabasi Mkoa wa Shinyanga kilichojengwa na Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV) na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kupitia Mradi wa Usafi wa Mazingira (WASH SDG).
Eneo la wanawake ndani ya Choo cha Kisasa cha umma katika Kituo cha Mabasi Mkoa wa Shinyanga kilichojengwa na Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV) na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kupitia Mradi wa Usafi wa Mazingira (WASH SDG).
Eneo la wanawake ndani ya Choo cha Kisasa cha umma katika Kituo cha Mabasi Mkoa wa Shinyanga kilichojengwa na Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV) na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kupitia Mradi wa Usafi wa Mazingira (WASH SDG).
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Jomaary Satura akizungumza wakati wa uzinduzi wa Choo cha Kisasa cha umma pamoja na Mtambo wa Gesi asilia (Bio – Gas Plant) katika Kituo cha Mabasi Mkoa wa Shinyanga vilivyojengwa na Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV) na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kupitia Mradi wa Usafi wa Mazingira (WASH SDG) na kufadhiliwa na Serikali ya Uholanzi.
Diwani wa Viti Maalumu Mhe. Shella Mshandete akizungumza wakati wa uzinduzi wa Choo cha Kisasa cha umma pamoja na Mtambo wa Gesi asilia (Bio – Gas Plant) katika Kituo cha Mabasi Mkoa wa Shinyanga vilivyojengwa na Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV) na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kupitia Mradi wa Usafi wa Mazingira (WASH SDG) na kufadhiliwa na Serikali ya Uholanzi.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Masumbuko akizungumza wakati wa uzinduzi wa Choo cha Kisasa cha umma pamoja na Mtambo wa Gesi asilia (Bio – Gas Plant) katika Kituo cha Mabasi Mkoa wa Shinyanga vilivyojengwa na Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV) na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kupitia Mradi wa Usafi wa Mazingira (WASH SDG) na kufadhiliwa na Serikali ya Uholanzi.
Katibu Tawala Wilaya ya Shinyanga Mhe. Boniphace Chambi akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko wakati wa uzinduzi wa Choo cha Kisasa cha umma pamoja na Mtambo wa Gesi asilia (Bio – Gas Plant) katika Kituo cha Mabasi Mkoa wa Shinyanga vilivyojengwa na Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV) na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kupitia Mradi wa Usafi wa Mazingira (WASH SDG) na kufadhiliwa na Serikali ya Uholanzi.
Katibu Tawala Wilaya ya Shinyanga Mhe. Boniphace Chambi akipanda mti kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko wakati wa uzinduzi wa Choo cha Kisasa cha umma pamoja na Mtambo wa Gesi asilia (Bio – Gas Plant) katika Kituo cha Mabasi Mkoa wa Shinyanga vilivyojengwa na Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV) na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kupitia Mradi wa Usafi wa Mazingira (WASH SDG) na kufadhiliwa na Serikali ya Uholanzi.
Katibu Tawala Wilaya ya Shinyanga Mhe. Boniphace Chambi akipiga picha ya kumbukumbu na viongozi wa Shirika la SNV, Manispaa ya Shinyanga na wadau wa afya na mazingira baada ya uzinduzi wa Choo cha Kisasa cha umma pamoja na Mtambo wa Gesi asilia (Bio – Gas Plant) katika Kituo cha Mabasi Mkoa wa Shinyanga vilivyojengwa na Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV) na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Katibu Tawala Wilaya ya Shinyanga Mhe. Boniphace Chambi akipiga picha ya kumbukumbu na Viongozi mbalimbali na wanafunzi wa shule ya msingi Ibinzamata baada ya uzinduzi wa Choo cha Kisasa cha umma pamoja na Mtambo wa Gesi asilia (Bio – Gas Plant) katika Kituo cha Mabasi Mkoa wa Shinyanga vilivyojengwa na Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV) na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Katibu Tawala Wilaya ya Shinyanga Mhe. Boniphace Chambi akipiga picha ya kumbukumbu na wadau katika kituo cha Mabasi Mkoa wa Shinyanga baada ya uzinduzi wa Choo cha Kisasa cha umma pamoja na Mtambo wa Gesi asilia (Bio – Gas Plant) katika Kituo cha Mabasi Mkoa wa Shinyanga vilivyojengwa na Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV) na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...