Na Jane Edward, Arusha

Tume ya Taifa ya Sayansi na teknolojia (Costech) imewakutanisha wanahabari na watafiti zaidi ya hamsini lengo likiwa ni kuwajengea uwezo waaandishi wa Habari kuandika habari za kisayansi na kirahisi

Kaimu Mkurugenzi Mkuu Costech Dkt Philbert Luhunga akifungua mafunzo hayo ya siku nne yaliyowaunganisha waandishi wa Habari kutoka Mikoa ya Arusha, kilimanjaro,Tanga na Manyara amesema mafunzo hayo yanalenga kuziba pengo kati ya waandishi, wahariri na Watafiti

Amesema kwa sasa waandishi wengi wamekuwa wakishindwa kutekeleza Majukumu yao kutokana na pengo la mawasiliano lililopo baina taasisi za kitafiti na waandishi wa Habari jambo linalosababisha waandishi kutotoa taarifa za Utafiti kwa wingi

"Hapa tumekuja kuwaunganisha waandishi wa Habari na watafiti ili waandishi muweze kuandika habari za kisayansi kwa wingi kutoka katika taasisi za kisayansi"Alifafanua.

Nao washiriki wa mafunzo hao Abraham Gwandu anasema kuwa mafunzo hayo yamekuwa muhimu sana kwa wanahabari na yataleta mabadiliko katika uandishi wa habari za kisayansi.

" Sisi kama waandishi Kwakweli tumekuwa nyuma kwenye kuripoti habari za kisayansi na sasa tunaendelea kupewa elimu kwahiyo tukitoka hapa tutajikita kwenye kuandika habari za sayansi kwa lugha rahisi inayoeleweka kwenye jamii"Alisema Gwandu

Kwa upande wake muwezeshaji wa mafunzo hayo Daktari Bakari Msangi anasema kuwa mafunzo haya ni kubadilishana uzoefu kati ya watafiti na waandishi lakini pia kufanya kazi pamoja katika masuala mbalimbali ya kitafiti na kuibua baadhi ya teknolojia ambazo zitakuwa na manufaa kwa Wananchi.

Kaimu Mkurugenzi wa Costech Philbert Luhunga akifungua mafunzo ya wanahabari na watafiti jijini Arusha

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...