Tarehe
 8 Machi kila mwaka ni siku ya Wanawake duniani ambapo siku hii 
inakumbusha na kutafakari juu ya matokeo ya Kijamii, Kisasa na Kiuchumi 
waliyofikia wanawake na msimamo wao imara katika ngazi ya kijamii kwa 
ujumla.
Katika
 kuadhimisha siku hiyo wanawake wa Mamlaka ya Majisafi na usafi wa 
Mazingira Dar es salaam (DAWASA) wameshiriki maadhimisho hayo 
yaliyofanyika katika viwanja vya Uhuru mkoani Dar es salaam huku kauli 
mbiu ya maadhimisho hayo kwa mwaka huu ni kizazi cha "Haki na ustawi kwa 
maendeleo endelevu"
Akizungumza
 kwenye maadhimisho hayo, Mkurugenzi wa Ukaguzi wa ndani DAWASA, CPA 
Rosemary Lyamuya amesema kuwa DAWASA inaadhimisha siku hii kwa mafanikio
 makubwa yaliyopatikana chini ya uongozi wa Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan
 kwani amewatua ndoo za maji Wanawake wa Jiji la Dar es salaam na Mkoa
 wa Pwani.
"Sisi
 kama Watumishi wanawake wa DAWASA tunampongeza Rais Samia Suluhu kwani 
maadhimisho haya yamekuwa ya mafanikio makubwa sana kwetu kwani 
utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Majisafi imewezesha kumtua mwanamke 
ndoo ya maji. Tumemtua mwanamke ndoo ya Maji maeneo mbalimbali kwa 
kukamilisha miradi ya Maji katika maeneo ya Kisarawe, Pugu, Chalinze, 
Mkuranga, Mbwawa ambayo kwa kiasi kikubwa imemuondolea mwanamke 
changamoto ya upatikanaji huduma."Alisema Rosemary
Ameongezea
 kuwa mafanikio yoyote yanayoonekana hapa Nchini na Duniani kote kwa 
kiasi kikubwa yamechagizwa na uwepo wa Wanawake katika nyadhifa kubwa na
 muhimu za kimaamuzi chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa 
Tanzania, Mhe. Samia Suluhu.
Baadhi
 ya Wanawake wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam 
(DAWASA) wakipita kwa mgeni rasmi Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam
 Bw. Hassan Rugwa wakati wa maadhimisho ya Siku ya wanawake duniani yaliyofanyika leo March 08, 2022 katika viwanja vya Uhuru jijini Dar es Salaam.
Baadhi
 ya Wanawake wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam 
(DAWASA) wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake Duninia 
yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Picha za pamoja


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...