Janeth Raphael - MichuziTv

MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka amewataka wanawake wa mkoa huo kujenga jamii yenye usawa ili watoto wa kike na kiume waweze kujisimamia katika maisha yao.

RC Mtaka amesema ni lazima wazazi wafundishe watoto wao masuala ya kijinsia ili kujenga jamii iliyo bora.

Mtaka ameyazungumza hayo  leo Machi 8, 2022 wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake  Duniani ambapo katika Mkoa wa Dodoma yalifanyika katika Wilaya ya Chemba.

Akizungumzia kuhusu manyanyaso ya wanawake katika jamii, RC Mtaka amesema ni lazima yaondolewe ili kusaidia wanawake kutekeleza majukumu yao katika jamii.

Pia, Mtaka ameongeza kuwa, Mkoa wa Dodoma utaandaa siku maalum kwa ajili ya kutambua wanawake wanaothubutu katika jamii ili waweze kutoa elimu ya mafanikio yao kwa wanawake wenzao.

Wakati huo huo, RC Mtaka pia amekabidhi vyeti vya pongezi na tuzo kwa watoto wa kike waliofanya vizuri darasani, wanawake mashuhuri na watoto waliofanya vizuri masomo ya Sayansi katika Chuo cha DECA.

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Neema Majule amewataka wanawake wasimame imara katika kufanya kazi. Amesema, wanawake wanaweza kufanya mabadiliko makubwa ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Munkunda amesema, wanawake waoneshe ulimwengu ujuzi wao kupitia fursa mbalimbali katika jamii.

"Wanawake tunaweza kufanya mambo makubwa kwa sababu sisi ni viongozi. Tukipewa kazi hatuharibu kwa sababu tumezaliwa kuwa viongozi," amesema Mkuu huyo wa wilaya.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya mwenyeji wa Chemba Saimon Chacha akizungumza kwa niaba ya wananchi wa Chemba amepongeza uongozi wa Mkoa wa Dodoma kwa kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani katika Wilaya ya Chemba.

Ameongeza kuwa, Halmashauri ya Chemba inatoa mikopo kwa wanawake pamoja na elimu ya mambo mbalimbali ili kuweza kuwasaidia wanawake  katika jamii.

Maadhimisho ya Siku ya Wanawake 2022 yamepambwa na kaulimbui isemayo "Kizazi cha Haki na Usawa kwa Maendeleo Endelevu".

MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka
Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mwanahamisi Munkunda wakati akizungumza jambo katika siku ya wanawake Duniani ikivyofanyika Wilayani chemba Mkoani Dodoma


Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Fatma Maganga akizungumza jambo




 Baadhi ya waandishi wa habari wananawake wa Mkoa wa Dodoma walioshiriki siku ya wanawake Duniani Kimkoa iliyofanyika Wilayani Chemba

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...